Habari za Punde

Rais Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi Atembelea Maonesho ya Kimataifa ya Tamasha la Pili la Utalii Zanzibar Viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar leo. WA

Rais Mstaaf wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwa na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombe, alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar leo kutembelea Maonesho ya Kimataifa ya Tamasha la Pili la Utalii Zanzibar.
Rais Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akizungumza na Mkurugenzi Masoko wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar.Dkt. Miraj, alipotembelea banda la maonesho la Kamisheni katika maonesho ya Tamasha la Pili la Utalii Zanzibar linalofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar. 
Rais Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi Masoko wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar.Dkt. Miraj akitowa maelezo ya picha katika mtandao wa Kamisheni ya Utalii unaoonesha sehemu mbalimbali za Jiji la Zanzibar na Vitongoji vyake katika Sekta ya Utalii Zanzibar.
Rais Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akitembelea banda la maonesho la MCL katika viwanja vya hoteli ya Verde, wakati wa Tamasha la Pili la Kimataifa la Utalii Zanzibar.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.