Mtawa wa Mtawa wa Shirika la Yesu Brother Vincent
Soleng (wa pili kushoto) akionesha Tuzo ya kutambua mchango wake katika
utunzaji mazingira kwa kupanda miti takriban 160,000 aliyopewa na Kiongozi wa
Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ambapo mgeni rasmi wa hafla hiyo alikuwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George
Simbachawene. Kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtakatifu Peter Claver, Padri
Karongo Buberwa.
Mtawa wa Mtawa wa Shirika la Yesu Brother Vincent
Soleng akitoa neno la shukrani katika hafla ya kumpongeza kwa kupewa Tuzo ya
Utunzaji mazingira na Papa Farncis.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. George Simbachawene akizungumza katika hafla ya kumpongeza
Mtawa wa Shirika la Yesu Brother Vincent Soleng mwenye umri wa miaka 83 ambaye
amepewa Tuzo na Kiongozi wa Kanisa Katiliki Duniani Papa Francis kutokana na
mchango wake katika utunzaji wa mazingira baada ya kupanda miti takriban
160,000 eneo la Ihumwa ilipo Shule ya Sekondari Mtakatifu PeterClaver Jijini
Dodoma.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtakatifu Peter Claver,
Padri Karongo Buberwa akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene kuzungumza.
Sehemu ya wanafunzi wa wa Shule ya Sekondari Mtakatifu
Peter Claver wakifuatilia matukio katika halfa ya kumpongeza Brother Vincent
Soleng.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtakatifu Peter Claver
wakitoa buridani katika hafla hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Mhe. George Simbachawene akipanda mti ikiwani sehemu ya kumuunga mkono Mtawa
Vincent Soleng aliyepanda miti laki sita katika eneo hilo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. George Simbachawene akiandaa sehemu ya kupanda mti ikiwa ni
sehemu ya kumuunga mkono Mtawa Vincent Soleng katika juhudi zake za utunzaji
mazingira.
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene (mbele katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma pamoja na wafanyakazi
wa Shule ya Sekondari Mtakatifu Peter Claver.
No comments:
Post a Comment