Habari za Punde

Digrii ya Kwanza ya Mwanafunzi Ndio Safari Yake ya Kwanza Inayotambulisha Usomi Wake.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wahitimu wa Kidato cha Sita, Walimu na Wiongozi wa Swizara ya Elimu wakati wa Hafla fupi ya kuwazawadia hapo Ukumbi wa Makonyo Wawi.

Na.Othman Khamis.OMPR.
Wahitimu waliomaliza masomo yao ya Kidato cha Sita Mwaka 2018 na kufaulu vyema daraja la Kwanza bado wana Kazi kubwa ya kujitafutia elimu zaidi katika njia ya kujijengea Maisha bora ndani ya mabadiliko ya sasa ya Teknolojia katika Maisha yao ya hapo baadae.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema hayo katika hafla fupi ya kuwazawadia Wanafunzi 33 waliomaliza Kitado cha Sita Mwaka 2018 na kuingia katika Wanafunzi Bora waliofanya vyema kwa kupata Daraja ya Kwanza hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.
Balozi Seif alisema mabadiliko yaliyopo Duniani hivi sasa yanayokwenda kwa kasi yanaonyesha na kuhesabu  kwamba Digirii ya Kwanza ya Mwanafunzi ndio safari yake ya kwanza inayomtambulisha usomi wake. Hivyo wahitimu hao wanalazimika kusoma kwa nguvu zao zote ili kuingia katika kundi hilo.
Aliwataka Wahitimu hao kuitumia vyema fursa waliyoipata ya kuendelea na msomo yao ya Vyuo kwa vile Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshajitolea kuendelea kujenga mazingira bora katika Sekta ya Elimu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaeleza Wahitimu hao kwamba Serikali bado inawajali Wanafunzi wake na ndio maana Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein hivi karibuni ameongeza fursa za udhamini kwa Wanafunzi wa 60 wa Waliofaulu Kidato cha Sita kuingia kazi ya Digirii.
Alisema kinachohitajika hivi sasa kwa Wanafunzi hao kuangalia masomo yanayouzika ili wamalizapo wasipate tatizo ya kupata ajira kwa vile kwa ajili ya elimu zao zitakuwepo za kutosha hasa fani ya Sayansi.
Balozi Seif alifahamisha kwamba Serikali imelazimika kuchukuwa Walimu wa Fani ya Sayansi kutoka Nchini Nigeria kuja kufundisha Visiwani Zanzibar kutokana na upungufu wa Walimu wenye Fani hiyo muhimu kwa maisha ya Ulimwengu wa sasa.
Aliwapongeza Walimu kwa kazi kubwa wanayoendelea kuitekeleza ya kuwafinyanga Wanafunzi wao Maskulini, kazi inayohitaji uvumilivu mkubwa kutokana na ugumu wake.
Akizungumza jukumu la Wazee kwa Watoto wao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka kuacha tabia ya kuwakatisha masomo yao kwa kuwaingiza katika ndoa mapema hasa wale wenye vipaji maalum.
Alisema Watoto wanastahiki kupata Haki yao ya Elimu hata kufikia Vyuo Vikuu kwa wale wenye uwezo huo na anapofikia hatua ya kumaliza suala la kuolewa litafuatia baadae wakati tayari ameshajengewa mazingira bora ya maisha yake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushukuru Uzalendo wa Mfanyabiashara Maarufu Nchini Said Nassir Nassor Bopar  unaoendelea kusaidia kuunga mkono Sekta ya Elimu hapa Nchini inayostahiki kuheshimiwa.
Balozi Seif alisema mchango wa Mfanyabiashara huyo kwa kuhamasisha Wanafunzi kutafuta elimu kwa njia zozote umewezesha chachu ya ongezeko la Ufaulu kwa Wanafunzi  katika Vidato mbali mbali Unguja na Pemba.
Mapema Mfanyabiashara Said Nassir Nassor {Bopar} alieleza kufarajika kwake na Heshima kubwa anayopewa na Viongozi wa Kitaifa, Walimu pamoja na Wananchi wa kawaida Heshima inayompa msukumo mkubwa wa kuendelea kuunga mkono Sekta za Kijamii ikiwemo Elimu.
Nd. Bopar alisema kutokana na ongezeko la ufaulu wa Wanafunzi hasa Kidato cha Sita na Nne amehamasika kuwapa zawadi maalum Wahitimu wa Vidato hivyo ili kuwaongezea motisha wa kuelekeza nguvu zaidi katika kujipatia Elimu ya juu.
Mfanyabiashara huyo Nchini ambaye amejitolea kutoa zawadi za Laptop, Mkoba pamoja na Bahasha  klwa Kila Mhitimu zilizojaa kisichofahamika kwa Wanafunzi wa Kike waliofanya vizuri na kuibuka Daraja la Kwanza katika Mitihani yao ya Kidato cha Sita Mwaka 2018.
Nd. Bopar ambae aliahidi kutoa Kompyuta Mbili kwa Kila Skuli iliyopasisha Wanafunzi hao aliahidi kuendelea kutoa zawadi kwa Wahitimu wa Mwakani hata kama kiwango cha ufaulu wao kitaongezeka na kufikia zaidi ya Wanafunzi 100 wa Daraja la Kwanza.
Akimkaribisha Mgeni zarsmi kutoa zawadi kwa Wahitimu hao wa Daraja la Kwanza waliomaliza  Kidato cha Sita Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma alisema Serikali kupitia Wizara hiyo itaendelea kushirikiana na Washirika wote katika kuona Sekta hiyo inazidi kuimarika zaidi.
Waziri Riziki aliendelea kuwaomba Wafanyabiashara wengine Nchini kuungana na Nd. Bopar alika kuwasaidia Wanafunzi wa Kidato cha Nne wanaojiandaa na Mitihani yao ambao kwa sasa wako Makambini.
Alisema Wanafunzi hao wanahitaji kusaidia huduma mbali mbali ili kuwapa utulivu utakaowajengea uwezo na nguvu zaidi za kuja kufanya vyema kwenye Mitihani yao ya Kitaifa Mwaka huu.
Jumla ya Wahitimu 34 wa Darala la Kwanza Kidato cha Sita wamekabidhiwa zawadi hizo ambao kati yao 33 wametoka Skuli za Sekondari za Serikali na Mmoja ametika Skuli Binafsi.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.