Habari za Punde

Kongamano la vijana kuhusu fursa za uchumi visiwani Zanzibar lafanyika



Mkuu wa Wilaya ya Kusini Idrisa Mustafa Kitwana akizungumza na Vijana wakati akifungua Kongamano la Vijana kuhusu fursa za kiuchumi visiwani Zanzibar huko katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar. 

 Mkurugenzi wa Masoko kutoka Kamisheni ya Utalii Dkt.Miraji Ussi akiwasilisha mada kuhusu Uchumi katika Sekta ya Utalii huko Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar katika Kongamano la Vijana .
 Kombo Dhikiri Kombo kutoka chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) akiuliza maswali kuhusu mada ya Uchumi Sekta ya Utalii katika  Kongamano la Vijana huko  Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar  .
icha ya pamoja akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kusini Idrisa Mustafa Kitwana wanne (kulia), Vijana na viongozi wengine kutoka Sekata mbali mbali.
Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.

NA Mwashungi Tahir    Maelezo      31-8-2019.
Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Idrissa Mustafa Kitwana  amewataka vijana nchini kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo visiwani  Zanzibar kwa lengo la kujitengenezea ajira  na kuacha kusubiria ajira kutoka Serikalini.
Akizungumza hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud huko katika Ukumbi wa Idriss Abdul-Wakil wakati wa kufungua Kongamano la vijana kuhusu fursa za kiuchumi zilizopo  visiwani Zanzibar.
“ Vijana ndio nguvu kazi ya Taifa katika kuinua uchumi nchini hivyo ni lazima mjikite katika kujituma wenyewe ili waweze kujipatia kipato cha halali,”alisema Mkuu wa Wilaya.
Amewataka vijana kizitumia fursa ziliopo katika kujiajiri wenyewe kwa kufanya kazi mbali mbali zenye kuwapatia rizki na kuacha kusubiria ajira kutoka Serikalini ikiwa Serikali haiwezi kuajiri vijana wote.
Aidha alisema ili vijana wawe na mustakabali mzuri wa  kukuza uchumi ndani ya nchi  na  kujiendeleza maisha yao   lazima wawe na elimu,wajiepushe na madawa ya kulevya ili Taifa liweze kuwa na  vijana wenye  afya bora na kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi .
“Elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo itumieni elimu kwa kuifanyia kazi mbali mbali ikiwemo ujasiriamali kilimo na sio kuweka vyeti ndani na kusubiri ajira wakati unakupiteni”, alisema Idrissa.
Akitoa wito kwa vijana  kuwataka kuhakikisha kongamano hilo litawajengea uwezo na wakitoka hapo waweze kubadilika kwa kuibua mambo mengi katika kujiongezea kipato chao.
Mh Idrissa amewataka vijana kuacha  kufikiria kwamba utalii ni kutembeza wageni tu ila kuna kazi nyingi ambazo ni za utamaduni wetu  ujasiriamali tukizifanya watalii watavutiwa nazo na pato litaingia nchini.
Nae Dkt Miraji Ussi Mkurugenzi Masoko Kamisheni ya Utalii   amesema Zanzibar utalii unakuwa   miradi mingi ipo ya kuvutia watalii ikiwemo spice, kusuka mikeka na mambo mengine vijana wafanye kazi hizo ili  kukuza uchumi.
Pia amesema  miradi mingine ni sekta ya malazi, bangaloo,  na michezo ya ngoma za kiasili  na mambo mengi ya Wazanzibar ambapo watalii huvutika nayo na kuwaomba vijana wachangamkie fursa hizo.
Wakitoa michango katika kongamano hilo Siti Hussein Jumamwanafunzi kutoka Skuli ya Benmbela  aliiomba Kamisheni ya Utalii kuwapangia sera maalum watalii wanapoingia nchini kuhusu suala la kivazi ili utamaduni wetu wetu uweze kuimarika .  
Kongamano hilo la siku moja mada nne ziliwasilishwa ikiwemo Ujasiriamali , Uchumi  sekta ya utalii, uchumi wa visiwani,na uchumi mafuta na gesi na kauli mbiu ya Kongamano hilo “TUMIA ELIMU KUWA FURSA YA MAENDELEO YA KIUCHUMI”.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.