Habari za Punde

SMZ Yatekeleza Ilani ya CCM Kwa Vitendo

Makamu Mwenyekiti Umoja wa Vijana wa CCM Taifa {UVCCM} Bi.Tabia Maulid Mwita akizungumza na Vijana wenye ulemavu pamoja na wazazi wao wakati akiwaaga wakijiandaa kuelekea nchini Misri kwa mafunzo ya Wiki Mbili hafla iliofanyika katika ukumbi wa CCM Afisi Kuu Kisiwandui.

Makamu Mwenyekiti Umoja wa Vijana wa CCM Taifa {UVCCM} Bi.Tabia Maulid Mwita  ameipongeza Ofisi ya Makamu wa pili kupitia idara ya watu wenye ulemavu kwa kuzithamini na kuzilinda haki za binadamu husuasan haki za watu wenye ulemavu.
Alisema Jamii imeshuhudia kila mara serikali ya mapinduzi Zanzibar ambayo inatekeleza kwa vitendo ilani ya CCM ikizingatia, kufuata miongozo na maazimio ya kimataifa katika kuridhia na kupisha sheria mbali mbali zinazowalinda watu wenye ulemavu kwa lengo la kuwajengea mazingira wezeshi.
Ndugu Tabia Maulid Mwita alieleza hayo wakati akizungumza na vijana wenye ulemavu pamoja na wazazi wao ikiwa ni sehemu ya kuwaaga kufuatia ziara yao ya kimafunzo  ya wiki mbili wakielekea nchini Misri hafla iliofanyika katika ukumbi wa CCM Afisi Kuu Kisiwandui.
Akizungumza na vijana hao amepongeza ushirikiano mzuri uliokuwepo kati ya serikali na taasis binafsi katika kuwatafutia fursa mbali mbali watu wenye ulemavu ikiwemo mafunzo nje ya nchi huku akiupongeza umoja wa watu wenye ulemavu Zanzibar (UWZ) kwa kuchangamkia fursa ya upatikanaji wa nafasi hizo kumi na mbili nchini Misri.
 Tabia Maulid Mwita aliwataka vijana hao wanaotarajia kwenda nchini Misri kuzingatia vyema na kwa makini mafunzo watakayopatiwa ili kuonesha utofauti baada ya kumaliza masomo yao na kuwa mabalozi wazuri katika kuwafundisha vijana wenzao wakati  watakaporejea Zanzibar.
“Nakuombeni sana mukifika huko muwe wanafunzi wazuri mtakaozingatia vyema mafunzo mtakayopatiwa ili mtakaporudi mje muwasidia na wenzenu” Alisisitiza Ndugu Tabia.
Alisema Chama cha Mapinduzi kitaendelea kuthamini haki za binadamu ikiwajumujisha watu wenye ulemavu kwani Ilani ya uchaguzi 2015-2020 imeweka wazi suala la kuwatambua na kuwawezesha watu walio katika makundi maalum.
Nae Mkurugenzi wa Idara ya watu wenye ulemavu Zanzibar Bi. Abeda Rashid aliwaomba vijana hao kushirikiana muda wote  watakapokuwa mafunzoni ili lengo lilokusudiwa liweze kufikiwa sambamba na kuwa wastahamilivu kwa yale mambo yote watakayokutana nayo katika kipindi chao cha masomo.
Mkurugenzi Abeda aliwatanabahisha vijana hao kutokana na mabadiliko na changamoto zinazojitokeza katika mataifa tofauti duniani kwa sasa itawabidi wawe waangalifu watakapokuwa safarini na kamwe wasikubali kumsaidia mzigo Mtu wasiyemfahamu kila watakapowasili katika viwanja vya ndege vya nchi jirani.
Katika hafla hiyo ya kuwaaga vijana hao Bi Abeda alisema katika jitihada za kuonesha serikali inawajali vijana wake Idara ya watu wenye ulemavu imetoa mchango utakaowasaidia wakiwa safarini angalau kuweza kujikimu kwa namna moja au nyengine.
Akitoa Shukrani kwa niaba ya wenzake Khamis Mwadini Khamis ameushukuru uongozi wa Chama cha Mapinduzi, Umoja wa watu wenye ulemavu na serikali kwa ujumla kwa msaada wao waliotoa katika kuwatafutia fursa na kuahidi kuwa watayazingatia yale yote waliYoelekezwa na watajitahidi kusoma kwa biidi ili kuendelea kujengia sifa Zanzibar.
Akizungumza kwa niaba ya umoja wa watu wenye ulemavu Bibi Salma Sadati alisema Uongozi umezingatia uwiano wa wilaya wakati wa kugawa nafasi hizo ambapo kundi la mwanzo la vijana hao linatarajiwa kuondoka Jumamosi ya tarehe 14 likifuatiwa na kundi jengine litakaloondoka Siku ya Jumapili Septemba 15 wakati wa Alfajiri.
Safari hiyo itajumuisha jumla ya vijana Kumi na Mbili (12),  wanawake wanane , na wanaume wanne  kati ya hao vijana wawili kutoka Kisiwani Pemba na wengine kutoka katika wilaya tofauti Kisiwani Unguja.
Khamis Mwadini Khamis Miongoni mwa Vijana waliobahatika kupata fursa ya masomo Nchini Misri akiutoa shukrani kwa niaba ya wenzake baada ya kupata fursa hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM.Bi.Tabia Maulid Mwita Kushoto akimpongeza Kijana Khamis Mwadini Khamis kuwa miongoni mwa Vijana waliobahatika kupata fursa ya masomo Nchini Misri.Kati kati yao ni Mkurugenzi wa Idara ya watu wenye ulemavu Zanzibar Bi. Abeda Rashid Abdullah.
Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.