Habari za Punde

Tanga Cement Kuazisha Timu ya Kampuni ya Mpira wa Miguu Miguu Itakayoleta Ushindani Nchini.

Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Tanga Cement Diana Malambugi akizungumza wakati akifungua mashindano ya Idara kwa mwaka 2019 yanayoendelea sambamba na wiki ya usalama Tanga Cement yanayofanyika kwenye viwanja vya Saruji Jijini Tanga Katika mchezo wa ufunguzi mabingwa watetezi timu ya WS Insight (Worriors) walicheza na timu ya Process ambapo mashindano hayo yamebeba ujumbe wa wiki ya Usalama Tanga Cement kwa mwaka 2019 ni Usalama wao, usalama wa familia yako.

KAMPUNI ya Saruji ya Tanga Cement imeweka bayana kwamba mipango yao ya baadae ni kuanzisha timu ya mpira wa miguu ambayo itakuwa bora lenye kuleta ushindani mkubwa kwa mkoa wa Tanga na Tanzania kwa ujumla.

Hayo yalisemwa leo na Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Tanga Cement Diana Malambugi wakati akifungua mashindano ya Idara kwa mwaka 2019 yanayoendelea sambamba na wiki ya usalama Tanga Cement yanayofanyika kwenye viwanja vya Saruji Jijini Tanga

Katika mchezo wa ufunguzi mabingwa watetezi timu ya WS Insight (Worriors) walicheza na timu ya Process ambapo mashindano hayo yamebeba ujumbe wa wiki ya Usalama Tanga Cement kwa mwaka 2019 ni Usalama wao, usalama wa familia yako.

Alisema lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kusaka vipaji na kupata timu ya kampuni ambayo itakuwa ni tishio kwa mkoa wa Tanga na kwenda kushiriki mashindano makubwa hapa nchini.

“Lakini pia kuweka wafanyakazi pamoja kupitia michezo hiyo kwa idara tofauti tofauti na hivyo kupelekea kukaa pamoja na kujua namna ya kushirikiana kuzidi kuongeza ufanisi “Alisema

Akizungumzia kuhusua mipango ya kushiriki Ligi kuu siku zijazo alisema ni lengo la mbali sana wameanza taratibu wanavyokwenda wale ambao wanaweza kuwasaidia wanaweza kuingia kuona namna ya kushirikiana nao

“Mashindano ya Riadha tumekuwa tukishiriki kila mwaka lakini hivi sasa tumechukua mtaalamu wa kuwafundisha ili wanapokwenda kwenye mashindano hayo wasiende kama wadhamini lakini pia washiriki na kushinda”Alisema

Hata hivyo alisema wakati utakapofika kwenye upande wa mpira wa miguu watasaka kocha ambaye atawafua mwaka mzima tungependa kufika huko lakini bado.

“Lakini pia tungependa hata kucheza na timu ya Coastal Union siku moja huku akieleza mashindano hayo walianza tokea 2016 na hasa zamani saruji walikuwa na timu nzuri sana kwenye michezo mbalimbali walikuwa na timu nzuri kwenye michezo mbalimbali na hata chimbuko la wafanyakazi wengi walikuwa wanakuja kutokana na michezo”Alisema

Alisema kwamba michezo ilikuwa imeimarika sana lakini miaka ya katikati ikafa na ilipofika 2016 wakaona warudishe michezo tararibu kwa kuwakutanisha wafanyakazi wao ili kuweza kuhakikisha wanatumia michezo hiyo kama sehemu ya kuimarisha afya zao . 

Awali akizungumza wakati wa mchezo huo Afisa Usalama wa Tanga Cement, Frank Ndalilo alisema kwamba wapo kwenye mashindano ya idara ambayo kampuni wameandaa watakakuwa wanashindana kwenye kuboresha afya.

Alisema kwamba mashindano hayo yanakwenda pamoja na wiki ya usalama kwao wameamua kuyaanzisha ili wafanyakazi watambue kwamba nini wajibu wao kwenye kazi na namna gani wanaweza kuhakikisha wanakuwa kazini wanalinda usalama wao ni mpango ambao umeanzishwa na kampuni hiyo. 

“Lakini mpaka sasa tunajivunia usalama ndani ya kiwanda unaendelea vizuri na wanaboresha usalama watu wafahamu mpaka sasa wanajivunia wamefikia masaa milio 5.278 pasipokuwa na ajali wala upotevu wa muda”Alisema.
 Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Tanga Cement Diana Malambugi akienda kukagua timu wakati akifungua mashindano ya Idara kwa mwaka 2019 yanayoendelea sambamba na wiki ya usalama Tanga Cement yanayofanyika kwenye viwanja vya Saruji Jijini Tanga
 Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Tanga Cement Diana Malambugi akipiga penati ikiwa ishara ya ufunguzi mashindano ya Idara kwa mwaka 2019 yanayoendelea sambamba na wiki ya usalama Tanga Cement yanayofanyika kwenye viwanja vya Saruji Jijini Tanga
  Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Tanga Cement Diana Malambugi akipiga penati ikiwa ishara ya ufunguzi mashindano ya Idara kwa mwaka 2019 yanayoendelea sambamba na wiki ya usalama Tanga Cement yanayofanyika kwenye viwanja vya Saruji Jijini Tanga
 Kikosi cha timu ya Process ambacho kilicheza na Wariors Securiy
 Kikosi cha timu ya Wariors Security

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.