Habari za Punde

Waziri MkuuMhe. Kassim Majaliwa Aaza Ziara Mkoani Geita,Akagua Ununuzi wa Zao la Pamba Chato.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nishati na Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Chato kuanza ziara ya kikazi mkoani Geita, Septemba 21, 2019. Kushoto na Waziri wa Madini, Doto Biteko na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Geita, Said Kalidushi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Chato kuanza ziara ya kikazi mkoani Geita, Septemba 21, 2019.Kulia ni Mkuu wa moa wa Geita, Mhadisi  Robert Gabriel  na kulia kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Nishati na Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kinu cha kuchambua pamba  wakati alipotembelea  Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Chama Kikuu cha  Ushirika cha Chato , Septemba 21, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati na mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel  na kulia ni Meneja   wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Chato, Charles Nyasi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama Pamba wakati alipotembelea maghala ya Kiwanda cha Kuchambua Pamba cha Chama  Kikuu cha Ushirika cha Chato mkoani Geita, Septemba 21, 2019. Kushoto ni Meneja wa Chama hicho, Charles Nyasi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Meneja  wa Chama Kikuu cha Ushirika la Chato, Charles Nyasi (kulia) wakati alipotembelea kiwanda cha kuchambua Pamba cha Chama hicho, Septemba 21, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel na wa pili kushoto ni Waziri wa Nishati na Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.