Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George
Simbachawene akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani
yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Na.Mwandishi.OMR.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. George Simbachawene amesema mabadiliko ya tabianchi nchi
huathiri moja kwa moja shughuli za kiuchumi na ustawi wa jamii hivyo huatarisha
amani.
Akizungumza kwenye kwenye Maadhimisho ya Siku ya Amani
Duniani yaliyofanyika Jijini Dodoma Septemba 21 Mhe. Simbachawene ambaye
alikuwa mgeni rasmi alisema kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabianchi
huchangiwa na shughuli za kibinadamu.
Alisema kuwa shughuli hizo husababisha kuongezeka kwa
halijoto, kupungua kwa kiwango cha mvua, kukauka kwa vyanzo vya maji na
kuongezeka kwa magonjwa ya binadamu, wanyama na mimea.
"Kwa kiasi kiasi kikubwa mabadiliko ya tabianchi
huchangiwa na shughuli za kibinadamu zikiwemo uchafuzi wa hali ya hewa,
uchomaji misitu, ukataji miti bila kuotesha na shughuli za kilimo na ufugaji
zisizozingatia uhifadhi wa mazingira ambazo huchangia kuongezeka kwa hali ya
joto," alisema Waziri huyo.
Aliongeza kuwa pamoja na athari za mabadiliko haya
kuzikumba nchi zote duniani pia huzikumbwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania
na hi ni kutokana na ukeli kuwa ukuaji wa uchumi wetu hutegemea zaidi shughuli
za kiuchumi.
Kutokana na hali hiyo Waziri huyo alibainisha kuwa ili
kukabiliana changamoto hizo kama nchi tunahitaji kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi ili kuhimili na kujiepusha na majanga yanayosababishwa nayo.
Alitahdharisha kuwa majanga yanayotokana na hali hiyo
husababisha hasara za kiuchumi na kijamii zinazochangia kuongezeka kwa umaskini
na hata migogoro ya kijamii.
"Chanzo cha kupotea kwa amani kwa baadhi ya maeneo
ni chanzo chake ni mabadiliko ya tabianchi na hali ikibadili watu wakakosa
mahitaji kama maji hawawezi kukubali kufa lazima watatumia nguvu yoyote kuyapata
kwa kugombana.
"Hali ya hewa ikibadilika kusababisha kukosekana
kwa maji watu watapambana na kutafuta yake kidogo yaliyopo na katika kuyatafuta
lazima watagombana hivyo kusababisha vurugu hivyo amani ina uhusiano mkubwa na
mabadiliko ya tabianchi," alisema.
Mhe. Simbachawene alidokeza kuwa Serikali inatambua
umuhimu wa mazingira hivyo imeendelea kufanya jitihada kubwa za kutunza na
kusimamia mazingira kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa ukuta wa
kingo za bahari.
Kwa upande mwingine Waziri Simbachawene alihimiza
jumuiya za kimataifa kuweka mkazo katika kukabiliana na janga la mabadiliko ya
tabia nchi kwa kuzingatia kuwa uchumi wetu hutegemea shughuli zitokanazo na
mazingira.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa
(UN)-Tanzania Amon Manyama alipongeza Serikali kwa jiihada zake za kulinda
amani hususana katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Alisema kuwa ni jambo jema kuchukua hatua madhubuti za
kukabiliana na changamoto hiyo na kuwa amani ni msingi wa kuanzishwa kwa UN
hivyo tuhakikishe jitihada hizi zinadumu.
No comments:
Post a Comment