Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Aendelea na Ziara Yake Pemba Atembelea Ujenzi wa Makazi ya Makamu wa Pili wac Rais wa Zanzibar.l

Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo Zanzibar Mzee Ramadhan China akimpatia Maelezo Balozi Seif  kuhusu maendeleo ya Ujenzi wa Nyumba za Makaazi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Kisiwani Pemba.
Na.OthmanKhamis.OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddia alisema wakati Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiendelea na mipango yake ya kuimarisha Viwanda  vidogo vidogo na vya kati, Wananchi wanapaswa kuchangamkia fursa zilizojitokeza katika kilimo cha Viungo ambacho bei yake kwa sasa imepanda Kimataifa.
Alisema wakati umefika kwa Rasilmali za Taifa zinazozalishwa Nchini zitumike kwa usimamizi wa Wataalamu Wazalendo kutengeneza bidhaa  kwenye Viwanda hivyo kupitia  viungo wanavyozalisha ili ziifaidishe jamii kiustawi na kuongeza mapato ya Taifa kwa ujumla.
Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo mwishoni mwa ziara yake ya Siku Nne Kisiwani Pemba kukagua Miradi mbali mbali  ya Maendeleo akianzia na shamba la Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Mtakata pamoja na kufahamu changamoto zinazokwaza ukamilishaji wa Miradi hiyo muhimu kwa ustawi wa Wananchi waliowengi.
Alisema Tanzania na Zanzibar kwa jumla kwa muda mrefu imekuwa ikisafirisha Rasilmali zake inazozalisha nje ya Nchi jambo ambalo hunufaisha ajira kwa Nchi hizo kitendo ambacho kinafaa kubadilishwa ili Rasilmali hiyo zianzie uchakachuaji wake hapa Nchini na baadae kusafirisha bidhaa kamili.
Balozi Seif alisema hakuna sababu kwa Wananchi na hasa Wakulima kulalamikia ajira wakati Serikali tayari imeshaweka mazingira mazuri ya mfumo wa upatikanaji wa fursa za kujiendeleza Kimaisha bila ya kusubiri ajira za Serikali ambazo zimepungua hivi sasa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimpongeza Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Balozi Amina Salum Ali kwa ushawishi wake mkubwa wa kusimamia ufufuaji wa Viwanda vilivyosimamisha uzalishaji na kuanzisha Viwanda Vipya.
Alisema jitihada za Waziri wa Biashara zimeitia moyo Serikali Kuu katika azma yake ya kuelekea kwenye Uchumiwa Viwanda ifikapo Mwaka 2025 ambao utasaidia kuongeza fursa za ajira hasa kwa Vijana na kupunguza Umaskini miongoi mwa Wananchi wake.
Naye kwa upande wake Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali alisema Wizara hiyo kupitia Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar {ZSTC}  inafanya mabadiliko makubwa kwenye Viwanda vyake ili viwe na uwezo mkubwa wa kuzalisha kwa kiwango na Tija.
Balozi Amina alisema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kuzingatia  ongezeko la bei kubwa kwa bidhaa zinazotokana na Viungo akitolea mfano vilimo vya  Mikaratusi, mchai chai, Mrehani na Mdalasini vinavyoweza kulimwa sehemu mbali mbali ya Ardhi ya Visiwa vya Unguja na Pemba.
Aliwahakikishia  Wananchi hasa Wakulima Nchini kwamba Vilimo hivyo vya Viungo  vina Bei kubwa  na ni vyema wakajenga utamaduni wa kuvilima hata pembezoni mwa Nyumba zao kwa Vile Serikali tayari imeshajizatiti kununua Rasilmali hiyo bila ya wasi wasi.
Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikagua  Bara bara inayoendelea kujengwa ya Gombani kupitia Pagali hadi Pondeani itakayojengwa kwa kiwango cha Lami, kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Nyumba ya Makaazi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar hapo Pagali.
Baadae Balozi Seif na msafara wake akapata wasaa wa kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Ghala Kuu la kuhifadhia  Dawa Kiswani Pemba linayojengwa katika eneo la Vitongoji Wawi Chake Chake.
Katika ukaguzi huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  alisisitiza haja ya Wahandisi na Wasimamizi wa Miradi hiyo kuhakikisha kwamba inakamilika kwa wakati kulingana na Mikataba ilivyosainiwa licha ya changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza.
Akitoa maelezo ya Ujenzi wa Ghala Kuu Kisiwani Pemba Mkurugenzi wa Bohari Kuu Zanzibar Nd. Zahran  Ali alisema Ujenzi wa Ghala hilo umezingatia vigezo pamoja na viwango vya Kimataifa vya uhifadhi wa Dawa.
Nd. Zahran alisema Jengo hilo litalogharimu jumla ya Shilingi Bilioni 1.8 tayari limeshafikia asilimia 42%  ya ujenzi wake  ambao kwa sasa bado umekabiliwa na changamoto ya vifaa vya kukamilisha ambavyo hupatikana nje ya Nchi.
Akizungumza na Viongozi wa Serikali, Siasa pamoja na Masheha wa Wilaya zote za pemba  katika mkutano wa majumuisho ya ziara yake hapo Ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi Chake Chake Balozi Seif aliwapongeza Masheha kwa Uzalendo wao wa kufichua mashamba ya Serikali yalio mikononi mwa baadhi ya Watu.
Balozi Seif alisema kazi kubwa iliyofanywa na Masheha hao itasaidia kuirahisishia Serikali Kuu kufanya uchambuzi wa kina katika kuweka utaratibu wa kudumu wa kuyaratibu Mashamba yake zikiwemo pia Eka Tatu walizopewa Wananchi kwa ajili ya shughuli zao za Kilimo kuendeleza Maisha yao ya kila siku.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea matumaini yake kwamba yale Mashamba yaliyokuwa bado hayajatambuliwa zaidi Mkoa wa Kaskazini Pemba jitihada zitaendelea kufanywa na Masheha wahusika ili atalazimika kurudi tena katika kipindi cha mwezi Mmoja kujiridhisha na utekelezaji wa kazi hiyo.
Wakichangia Mkutano huo baadhi ya Masheha kutoka Shehia 129 za Wilaya Nne Kisiwani Pemba walielezea masikitiko yao kutokana na changamoto kubwa walizopambana nazo katika zoezi la utafutaji wa Mashamba ya Serikali katika Shehia zao.
Walizielezea changamoto hizo kuwa na pamoja na tuhuma zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya Watu kwamba Masheha walihusika katika kuficha Mashamba tuhuma ambazo zinavunja moyo kwa vile wao ndio waliohusika kufichupia pia Mashamba ya ziada ambayo hayakuorodheshwa ndani ya Daftari la linalotumiwa.
Walisema wimbi la ujenzi holela katika Eka za Serikali, uuzaji wa baadhi ya Mashamba hayo kinyume na Utaratibu, baadhi ya Watu kumiliki Eka zaidi sita pamoja na uvamizi wa eka zilizokuwa chini ya usimamizi wa baadhi ya Watu waliof ariki Dunia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.