Na Khadija Khamis – Maelezo Zanzibar 22/11/2019
MWENYEKITI wa Baraza la Vijana Taifa Khamis Haji Kheir ( Makoti) amewataka vijana kubuni miradi mbali mbali ya maendeleo katika Wilaya zao ili kupunguza changamoto za ajira nchini.
Akizungumza katika mkutano wa utekelezaji wa kazi za Baraza la Vijana pamoja na kujadili ajenda ya kikao cha baraza la watendaji,kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mkutano wa Baraza la Utamaduni Mwanakwerekwe.
Alisema vijana wachangamkie fursa zilizopo katika Wilaya zao kwani kufanya hivyo kutawasaidia kupata ajira na kuondokana na utegemezi wa ajira Serikali.
“Vijana lazima wachangamke kutafuta mbinu za kubuni miradi na wasikate tamaa na hili Serikali ipo tayari kuwaunga mkono katika harakati za kujiinua kiuchumi.” alisema Mwenyekiti .
Hata hivyo alisema Serikali kupitia Baraza la vijana linawasimamia vijana hao zaidi ya 150 kwa kila wilaya kuwapatia mafunzo ya ufundi na kuwaongezea ujuzi, uweledi kwalengo la kupunguza ukali wa maisha.
Aidha alisema Makoti kuna baadhi ya viongozi wa shehia na Wilaya wamechaguliwa kwa kutekeleza majukumu ya kuwasimamia vijana katika kubuni miradi lakini hutoa visingizio vya kutosaidiwa na baraza na Serikali , hivyo hukaa bila ya kufanya kazi yeyote jambo ambalo linazorotesha maendeleo.
‘’Kwa mtu ambaye amechanguliwa kuwa kiongozi wa baraza la vijana ambae kazi yake ni kuwasimamia na kuwasaidia vijana angalie majukumu yake ya kazi na kuacha kutoa visingizio visivyokuwa na msingi.”alisema Makoti
Alisema katika kuhakikisha baraza linasonga mbele limepanga mikakati ya kusimamia vijana kwa kuwaimarisha,katika mafunzo mbali mbali ya ufundi kushirikiana na Serikali ili kufikia malengo ya kuwapatia maendeleo vijana katika nyanja ya kijamii na kiuchumi.
Nae Ofisa Mratibu wa Baraza la Vijana Salum Issa Ameir aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi kujiunga na mabaraza hayo ili kupata fursa mbali mbali zinazojitokeza ikiwemo mafunzo ya ufundi na miradi ya kimaendeleo.
Kikao hicho kilihusisha vipengele tofauti vya utekelezaji wa baraza hilo ikiwemo ushauri, mipango ya ajira kwa vijana,pamoja na kuyaimarisha mabaraza ya vijana Wilaya Shehia na hadi Taifa A
No comments:
Post a Comment