Habari za Punde

Mkutano wa SADC wa Wataalamu wa Utatu Sekta ya Kazi na Ajira

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akizungumza na wataalamu wa sekta ya kazi na ajira wakati wa mkutano uliowakutanisha Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupitia na kujadili ajenda mbalimbali zinazohusu sekta hiyo.
Sehemu ya Wataalamu wa Sekta ya Kazi na Ajira kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilisha katika mkutano huo uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa sekretarieti ya SADC, Bw. Maxwell Parakokwa (kushuto) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo uliowakutanisha wataalamu wa utatu wa sekta ya kazi na ajira Novemba 20, 2019 Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe na Mkurugenzi wa Huduma za Kijamii na Rasilimali Watu SADC, Bi. Duduzile Simelane (katikati).
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakisikiliza mada zilizokuwa zikiwasilisha kuhusu sekta ya Kazi na Ajira.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wazee, Wanawake na Watoto Zanzibar Bi. Fatma Bilali wakati wa mkutano wa wataalamu wa sekta ya kazi na ajira.
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Willington Chibebe akieleza jambo kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe wakati wa mkutano wa wataalamu wa sekta ya kazi na ajira uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu 
(Kazi,Vijana na Ajira na Wenye Ulemavu.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.