Na. Abdi Suleiman - Pemba.
MENEJA wa
Pataya Guest house ya Machomanne Chake Chake Pemba, Said Seif Said amesema kuwa
anatowa wiki moja kwa shirikisho la Mpira Zanzibar (ZFF), kumlipa fedha zake za
waamuzi waliokuwa wakilala katika hoteli hiyo, vyenginevyo anakwenda kwenye
vyombo vya sheria kudai haki yake.
Said alisema kuwa wiki hiyo ni kuanzia Disemba 29 mwaka 2019,
ikipita atakipeleka chama hicho katika vyombo vya dola kwa kudai malipo ya
waamuzi hao, kwani ni miezi mingi imepita bila ya kupata haki yake licha ya
kuwasiliana na viongozi wakuu wa chama hicho.
Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi
wa habari za michezo, katika ofisi za gesti hiyo iliyopo mtaa wa machomanne
Chake Chake Pemba.
Aidha meneja huyo aliwataja waamuzi hao, ambao wamelala na
kutokulipwa fedha zake kiasi cha shilingi laki 315000 kwa siku tisa ambacho
chumba kwa siku ni shilingi 35000, kuwa ni Mfaume Ali, Mohd Mwalim, Mbaraka
Haule na Issa Haji.
Alisema dhamana ya malipo ya waamuzi alikubaliana na
Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi Kibabu Haji, juu ya malipo na mwanzo walipokuwa
wakilala walikwenda vizuri, baadae ndio maharibiko yalipoanza pale walipokuwa
wakilala siku tano wanalipwa tatu na mwisho hajalipwa kabisa.
"Ndugu waandishi kama hawajinipa pesa zangu na hali
ikaendelea kuwa hivi, mimi nitaenda kwenye vyombo vya sheria kudai haki yangu,
nimeshadai sana na hakuna linaloendelea mpaka sasa" alisema.
“Mwanzo walikaa siku Tanoa wakalipa siku tatu, halafu wakaa
siku mbili, hawakuliza zikawa siku nne, halafu wakaja tena wakakaa siku tano,
zitakuwa siku Tisa na wanakuja waamuzi wawili wawili, zote hizo mimi sijalipwa
mpaka sasa’alisema.
Aidha alisema tayari jutihada mbali mbali alishazifanya,
ikiwemo kuwasiliana na wahusika juu ya kupata haki yake, lakini mpaka sasa
hakuna jibu sahihi juu madai yake kupatiwa.
Said alifahamisha jitihada nyengine alizichukuwa kwa
kuwasiliana na rais wa chama hicho, kwa njia ya ujumbe mfupi wa sms baada ya
kuona simu haipokeliwi, jambo ambalo limemrudisha nyuma kimaendeleo ikizingatiwa
mwanzo walikubalia vizuri juu ya malipo.
Hata hivyo alisema kibaya zaidi fedha hizo ni fedha za taasisi
ambayo inalipa Kodi, zinatumika kwa ajili ya kuendeshea shuhuli na sio
kuishia mikononi mwa mtu au taasisi.
Katibu wa shirikisho la soka Zanzibar (ZFF) Mohamed Ali
Hilali (Tedy), alikiri kulifahamu deni hilo huku akiahidi kuwa uongozi
utahakikisha unalilipa haraka iwezekanavyo.
Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi Zanzibar, ambaye pia ndie
aliekuwa akichukuwa dhamana ya malipo ya waamuzi hao, Kibabu Haji akiri
kulifahamu deni hilo na kudai kuwa tayari alishaliwasilisha katika chama husika
kwa ajili ya utekelezaji.
Alisema yeye jambo hilo sio la kwake bali ni la taasisi
husika, hivyo majukumu yake ya kiutendaji baada ya kumaliza aliliwasilisha kwa
uongozi, kwani hata wakati akipatiwa malipo yake huko mwanzo taarifa zilifika
kwa wahusika.
“Baada ya kupatiwa malipo yake huko mwanzoni pia stakabadhi
za malipo aliweza kutoa, hicho ambacho hakikupatikana nilitoa muongozo wote ili
kupatiwa haki zake”alisema kibabu.
Hata hivyo alimtaka Mmiliki huyo kuendelea kuwasilina na
viongozi wajuu wa soka ili kuona haki zake anapatiwa kwa njia gani, kuliko
kukimbilia kwenye vyombo vya sheria.
No comments:
Post a Comment