Habari za Punde

Jumla ya Wafungwa 79 Waachiwa Huru Katika Gereza la Butimba Mkoani Mwanza Mara Baada ya Kupewa Msamaha wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza CGP Phaustine Kasike wakati wakisimamia zoezi la kuachilia huru wafungwa 79 katika Gereza la Butimba kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutoa msamaha huo jana katika sherehe za Uhuru.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza CGP Phaustine Kasike wakati wakisimamia zoezi la kuachilia huru wafungwa 79 katika Gereza la Butimba kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutoa msamaha huo jana katika sherehe za Uhuru.Mkuu wa Gereza Kuu la Butimba ACP Shaku Umba akimkabidhi fedha za nauli Lucas Mwita mwenyeji wa Tarime mkoa wa Mara ambaye alikuwa ni mmoja wa wanufaika wa Msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alioutoa siku ya jana. Mzee Mwita ametumikia jumla ya miaka 20 katika Gereza hilo la Butimba.Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza CGP Phaustine Kasike akiwa pamoja na Mkuu wa Gereza Kuu la Butimba ACP Shaku Umba wakisalimiana na Wafungwa wanawake waliobahatika kupata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alioutoa jana wakati wa Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Jumla ya Wafungwa 79 wameachiwa huru katika Gereza hilo. 
Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.