Habari za Punde

Walimu Watakiwa Kuwafuatilia na Kuwalinda Watoto na Vitendo Vya Udhalilishaji.

Na. Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.
Wazazi na Walezi Nchini wametakiwa kushirikiana na Serikali katika kupiga vita vitendo vya udhalilishaji zidi ya Watoto ambavyo vimekithiri katika Jamii,
Hayo ameyasema Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Hassan Khatibu Hassan huko Ukumbi wa Amani Mkoa wakati akizungumza katika Mahafali ya tatu ya Skuli ya Farhiya iliopo Mwera Mtofaani wilaya ya Magharibi A.
Amesema licha ya Serikali kupambana katika kupiga vita vitendo vya udhalilishaji Wazazi pia wawe na mchango mkubwa katika vitendo hivyo ili kuweza kuwanusuru watoto na janga zito linaloendelea kuongoza hivi sasa  ndani ya jamii.
Aidha amesema amefurahishwa na juhudi za Walimu wa Skuli hiyo katika kuhahakikisha wanawajenga Wanafunzi ili  kufanya vizuri katika masomo yao  waweze kuwa  wataalamu bora hapo baadae,
Vile vile amewataka Walimu wasitosheke na kiwango walichofikia cha elimu badala yake wajitahidi kuwafundisha watoto hasa masomo ya Ujasiriamali ili waweze kujiajiri baada ya kumaliza mitihani yao.
Amewataka Walimu na Wazazi kushirikiana katika kuhakikisha wanawalinda na kuwafatilia watoto ili waweze kunusurika na vitendo vya udhalilishaji   pia wahamasike katika  masomo yao na wafikie malengo waliojiwekea.
Hata hivyo wanafunzi wametakiwa kujitahidi katika kufatilia masomo yao ili waweze kafanya vizuri  mitihani  na wathamini nguvu za wazazi wao na Serekali kwa  jumla.
K wa upande  wa  risala yao  wanafunzi hao wamesema katika mafanikio waliyoyapata  ni pamoja na  usomeshwaji wa ngazi ya Maandalizi  mpaka kufikia ngazi ya msingi kwa lengo la kuengeza elimu na kutarajia kufika  hadi Chuo.
 Wameelezea changamoto zao  mbalimbali kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi  ambazo zinawakabili ni pamoja na  upungufu wa maji safi ,Fotokopi,Printa na komputa.
Pia wameiomba Serikali kuwasaidia na kuwatatulia changamoto walizo nazo ili waweze kupata elimu yenye ubora  na kuhakikisha wanafikia malengo yao walojipangia hapo baadae ya kuweza kujiimarisha katika maisha yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.