Na. Kijakazi Abdalla.
Mfuko wa Hifadhi Zanzibar (ZSSF) umekabidhi msaada wa mabati 50 kwa Skuli ya na Maandalizi Mwembeshauri kwa ajili ya kuezekea banda la skuli hiyo.
Akikabidhi msaada huo Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya (ZSSF) Ali Suleiman Ahmada amesema kuwa msaada huo ni kwa ajili ya ujenzi wa darasa la Skuli ambalo linavuja.
Amesema kuwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) umekabidhi msaada huo baada ya kupata maombi kutoka kwa Muakilishi wa Jimbo hilo Nassor Salum Jazeera wa kutaka kusaidia mabati .
Aidha amesema kuwa lengo la mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) ni kurejesha huduma kwa jamii ili kuona mfuko huo unawanufaisha wananchi wake katika Nyanja za elimu pamoja na afya.
Hata hivyo ameitaka jamii kuzidisha nguvu zaidi katika kuchangia katika mfuko huo ili kuwekeza kwani kuekeza ni moja ya kujiekea nguvu hapo baadae
Nae Mwalimu Msaidizi wa Skuli ya Mwembeshauri Mgeni Rajabu Khamis ameushukuru Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) kwa msaada walioutoa kwani umekuja kipindi muafaka.
Aidha amesema kuwa msaada huo utazidisha nguvu kwa walimu ya kujenga ari ya ufundishaji kwa kuwapatia wanafunzi elimu bora ambayo inahitajika katika skuli hiyo.
“Msaada umekuja kipindi muafaka utatuzidishia nguvu zaidi ya kufundisha na wanafunzi watasoma katika mazingira yaliyo bora”alisema Mwalimu Mgeni.
Nae Muakishi wa Jimbo la Kikwajuni Nassor (Jazeera) ameitaka jamii kuzidisha nguvu za kuchangia mfuko huo ili kupata manufaa hapo baadae
Aidha amezitaka taasisi nyengine wajitokeze kuiga mfano kama huo wa kusaidia jamii hasa katika Nyanja ya elimu kwani kuekeza katika njia moja ya kujiengezea uwezo.
No comments:
Post a Comment