Habari za Punde

Dk. Mwinyi Afungua Bwalo la Maofisa wa JKU Dunga Wilaya ya Kati Unguja.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.Mhe.Dk.Hussein Mwinyi akiondoa kipazia kuashiria ufunguzi wa jengo la Bwalo la Maafisa wa Chuo cha Uongozi cha JKU Dunga Wilaya ya Kati Unguja ikiwa ni shamrashamra za kuadhiumisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, hafla hiyo imewfanyika katika eneo la Chuo hicho huku Dunga.


Na.Rahma  Khamis –Maelezo Zanzibar. 09/01/2019
Waziri wa Ulinzi wa Jeshi la Kujenga Taifa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hussein Ali Hassan Mwinyi amelitaka Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) kuimarisha nidhamu ya kazi ili kupata jeshi imara lenye utendaji bora Nchini .

Wito huo ameutoa katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU)  Dunga Wilaya ya Kati Unguja wakati akizinduwa Jengo la  wa Bwalo la Maafisa na Wapiganaji wa jeshi hilo.
Amesema ni jukumu la Jeshi hilo kuwalea vijana katika maadili mema ya kazi ili kuweza kuwajengea uwezo wa utendaji wa kazi  zao .
Aidha amefahamisha kuwa Jeshi litoe mafunzo mbalimbali kwa vijana wao ili kuongeza  uzalishaji mali katika miradi ambayo itasaidia kuengeza pato la Taifa .
Waziri Mwinyihaji amelitaka Jeshi la kujenga uchumi (JKU) kushirikiana  pamoja na  Jeshi la kujenga Taifa (JKT)kwa kuweza kutembelea na kubadilishana uzoefu katika kazi zao.
Nae Naibu Katibu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Sida Mohammed Himid amesema Ujenzi wa Bwalo hilo ni muendelezo wa ujenzi wa nyumba za kisasa ikiwa ni miongoni mwa Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi .
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar Kanal Ali Mtumweni Hamadi  amesema kufanikisha ujenzi wa bwalo hilo kutasaidia kuimarisha Maofisa na Wapiganaji wa jeshi hili kupata mapumziko ya kujenga mawazo mampya ya kiutendaji kwa kupata nafasi ya kubadilishana mawazo yao pamoja .
Kwa Upande wa  Katibu Mkuu wa  Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa na Idara Maalum za SMZ Sida Mohamed Hemed amesema  utekelezaji wa majukumu ya kimaendeleo katika jeshi hilo  wameweza kujenga Skuli ya Sekondari ya Mtoni pamoja na Skuli ya Ufundi Mtoni  .
Alisema waliweza kukarabati Majengo ya kambi mabwalo na   sehemu mbalimbali za jeshi hilo kwa Unguja na Pemba.
Alieleza kuwa Sambamba na hayo wanatarajia kuweka mikakati ya kujenga Mabwalo manane na vituo vya afya sita katika kambi za Unguja na Pemba .
Hata hivyo  Katibu huyo alieleza changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa ujenzi wao ni uhaba wa rasilimali ya mchanga pamoja na kupanda gharama za vifaa vya ujenzi  zinachangia kuzorotesha ufanisi wa kazi zao .
 Mradi wa Ujenzi wa Bwalo la Maafisa na Wapiganaji limegharimu jumla ya shilingi milioni 41 za kitanzaniaambalo lilisimamiwa na Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar. 
Mkuu wa Kambi ya Dunga Meja.Khadija Ahmada Rai akimpa maelezo  juu ya Bwalo la Maafisa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Hussein Ali Mwinyi kuhusiana na ujenzi wa Bwalo hilo.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.