Katika salamu hizo za rambirambi, Rais Dk. Shein
alieleza kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Sultan Qaboos
bin Said Al Said aliyefariki Januri 10, 2020 akwia na umri wa miaka 79.
Salamu hizo ziliendelea kuweleza kuwa kwa niaba ya wananchi, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na
yeye mwenyewe binafsi, Rais Dk. Shein anatuma salamu za rambi rambi kwa serikali,
familia pamoja na ndugu jamaa pamoja na wananchi wote wa Oman kufuatia kifo cha
kiongozi wao huyo.
Aidha, salamu hizo ziliongeza kuwa wananchi wa
Zanzibar wanaungana na ndugu zao wa Oman katika msiba huo mzito wa kiongozi
huyo na kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Sultan Qaboos mahala
pema peponi,Amin.
Sambamba na hayo, salamu hizo zilieleza kuwa kumbukumbu
ya mafanikio na mchango mkubwa alioutoa Sultan Qaboos katika maendeleo ya Oman
na duniani kwa jumla yataendelea kukumbukwa daima kwa Oman pamoja na wapenda
amani wote duniani.
“Namuomba Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira ndugu,
jamaa, wanafamilia na wananchi wote wa Oman katika kipindi hichi kigumu cha
msiba”, ilieleza sehemu ya taarifa hiyo ya rambirambi aliyoituma Rais Dk. Shein.
Sultan Haitham Bin Tariq Al Said ambaye alikuwa
Waziri wa Utamaduni na thurathi za kitaifa ameapishwa siku ya Jumaamosi baada
ya mkutano wa Baraza la Familia ya Kifalme kuwa mrithi wa Sultan Qaboos.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment