Habari za Punde

Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar Yawasilisha Utekelezaji Mpango Kazi Kuazia Mwezi wa Julai Hadi Disemba 2019 /2020

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Hamad Rashid Mohammed akiwasilisha muktasari wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa wizara yake kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019/2020, mkutano huo umeongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo pichani) (kushoto kwa Waziri) Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na kulia Mshauri wa Wizara ya Afya Zanzibar Dr. Jidawi, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.17-2-2020.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiongoza mkutano wake na Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, (kulia kwa Rais) Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi.Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee, Waziri wa Afya Zanzibar.Mhe.Hamad Rashid Mohammed na Mshauri wa Wizara ya Afya Dr. Jidawi.  

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Ali Abdalla akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji ya Mpango Kazi ya Wizara yake kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 /2020, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Maofisa wa Idara mbalimbali za Wizara ya Afya Zanzibar wakifuatilia Taarifa ya Utekelezaji ya Mpango Kazi wa Wizara yao wakati ikiwasilishwa na Katibu Mkuu Bi Asha Ali Abdalla, (hayupo pichani) mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee akiuliza swali wakati wa mkutano wa kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Afya Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. (kulia) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Hamad Rashid Mohammed na Mshauri wa Wizara ya Afya
 Dr. Jidawi.  
Mfamiasia Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Habib Ali Sharif akichangia wakati wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Afya kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 /2020, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Maofisa wa Wizara ya Afya kutoka Idara za Wizara hiyo wakifuatilia Taarifa hiyo ikiwasilisha katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Madaktari na Maofisa wa Wizara ya Afya kutoka Idara za Wizara hiyo wakifuatilia Taarifa hiyo ikiwasilisha katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.