Habari za Punde

Italia yaongoza uingizaji Watalii Zanzibar

Afisa Takwimu Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Raya Mohmed Mahfudhi akitoa Takwimu za uingiaji wa wageni kwa mwezi Januari 2020 imeonesha kupanda kwa wageni 58,761 sawa na ongezeko la asilimia 27.4 ikilinganishwa na wageni 46,133 walioingia  mwezi Januari 2019, hafla iliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini Mjini Zanzibar.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Takwimu za uingiaji wa wageni (watalii) kwa kwaka 2020 wakifuatilia tarifa ya takwimu hizo.
  Muandishi wa habari kutoka Dailynews Issa Yusuf akiuliza maswali katika Mkutano wa Takwimu za uingiaji wa wageni Nichini kwa mwaka 2020. Hafla iliyofanyika Ofisi za Mtakwimu Mkuu wa Serekali Mazizini Mjni Zanzibar.
Mkuu wa Kitengo cha Takwimu za Utalii Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serekali Abdulmalik Bakari Ali akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wandishi wa habari.
Picha na Makame Mshenga.
Na Mwashungi Tahir          Maelezo     18-2-2020.
Imeelezwa kwamba idadi walioingia nchini kwa mwezi wa January 2020 ni 58.761 sawa na ongezeko la asilimia 27.4 ikilinganishwa  na wageni 46,133 walioingia  mwezi wa January mwaka 2019.
Hayo amewasilisha  Raya Mohammed Mahfoudh Afisa Takwimu Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali  huko katika Ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu wa Serikali  uliopo Mazizini wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uingiaji wa wageni Zanzibar.
Amesema Nchi inayoongoza kuleta wageni ni Italia ambapo jumla ya wageni 8,903 asilimia 15.2 waliwasili Zanzibar , ikifuatiwa na Ufaransa asilimia 7.8 na Marekani asilimia 5.7
Pia amesema kwa upande wa Bara la Ulaya  asilimia 67.7 ya wageni walioingia mwezi wa January 2020  ambapo sawa na ongezeko la asilimia27.2 ikilinganishwa na mwezi wa January mwaka 2019.
Aidha amesema wageni 28,634 waliongia nchini ni wanaume  na wageni 30,127 ni wanawake  ambapo asilimia 5,2 ya wageni walikuwa na umri chini ya miaka 15, asilimia 86.2 ni wenye umri wa miaka 15-64 na asilimia 8.6 ni wenye umri kuanzia miaka 65+.
Kwa upande wake Kamisheni ya Utalii Afisa Masoko Maabadi Jaffar Muhidini amesema sababu  zinazopelekea kuongezeka wageni Zanzibar ni pamoja  na kuwepo vivutio vingi vya kutembelea wageni na kuwepo kwa amani na utulivu .
Pia alisema sababu nyengine ni kuwepo kwa hoteli kubwa kama vile Park Hayat , Serena na vile vile wataliana ndio wa mwanzo kutembelea Zanzibar hasa sehemu za Kaskazini Kiwengwa ambapo kuna hoteli nyingi za kisasa.
Nae Abdul-malik Bakari Ali Mkuu wa Kitengo cha Takwimu za Utalii Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali amesema  taarifa hizo zinapatikana kila mwezi kutokana na ukusanyaji wa wageni nchini na kuhakikisha jamii wanazipata kwa uhakika jinsi ya uingiaji wa wageni hao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.