Habari za Punde

Mkutano wa Kwanza wa SADC Kufanyika Zanzibar wa Kamati ya Mawaziri Wenye Dhamana ya Masuala ya Kukabiliana na Maafa wa SADC.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Raisi Mhe.Mohammed Aboud Mohammed akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya kukabiliana na Maafa wa Jumuiya ya MaendeIeo Kusini mwa Afrika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Mnazi mmoja .
Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Makame Khatibu Makame akitoa Ufafanuzi kwa Waandishi wa Habari kuhusu masuali ya maafa katika  Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya kukabiliana na Maafa wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika huko Ukumbi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Mnazi mmoja .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Raisi Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya kukabiliana na Maafa wa Jumuiya ya MaendeIeo Kusini mwa Afrika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Mnazi mmoja .
Na Khadija Khamis Maelezo Zanzibar   16/02/2020
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed amesema Mkutano wa  Kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Kukabiliana na Maafa  wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unatarajiwa kufanyika Zanzibar katika Hoteli ya Madinat al Bahr   tarehe 18 mwezi huu .
Hayo ameyasema huko katika Ukumbi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ( ZBC. TV) Mnazimmoja wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali viliopo Zanzibar .
Amesema Mkutano huo unafanyika kutokana na umuhimu mkubwa wa Mawaziri wa nchi Wanachama wa SADC  wanaohusiana na masuala ya Maafa kuweza  kukutana pamoja  kwa lengo la kujadiliana na kuweka mikakati ya namna bora ya kukabiliana na matukio ya maafa yanayoukabili Ukanda wa Kusini mwa Afrika .
Aidha amesema Mkutano huo wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika unalengo la kushajihishaji juhudi zilizopo katika kukabiliana na maafa kwa kuziwezesha nchi wanachama kuandaa mikakati ya uhimili kutokana na athari za Maafa.
“Adhari za maafa ni ukame mafuriko maradhi ya mripuko na mengineyo ambayo hutokezea kutoka na hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi na kuharibu miundombinu mbali mbali ikiwemo barabara na huduma za msingi za jamii”,  alisema Waziri Aboud
Alifahamisha kuwa mikakati hiyo itasaidia kupunguza athari za maafa na kuimarisha uwezo wa nchi husika katika kukabiliana na maafa pamoja na kurejesha hali baada ya maafa kutokea.
Alieleza kuwa SADC imetekeleza program ya ufanyaji wa tathmini na uchambuzi wa usalama wa chakula kwa nchi wanachama 14 zilizoathiriwa na majanga yanayotokana na hali ya hewa yakiwemo ukame na kuandaa mpango mkakati wa pamoja kwa ajili ya kujikinga .
Alisema mikakati hiyo ni kwa ajili ya kupunguza athari za maafa mnamo mwaka 2017 hadi 2018 takriban watu wapatao milioni saba waliathiriwa na maafa idadi ambayo ni ndogo ikilinganishwa na watu milioni 17 walioathirika katika miaka 2015-2016.
Waziri Aboud alisema mkutano  huu wa Kamati ya Mawaziri wenye thamana ya masuala ya Kukabiliana na Maafa  wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC) ni fursa tosha ya kutangaza utalii na kukuza uchumi wa nchi pamoja na kupunguza athari za Maafa Nchini .
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Makame Khatibu Makame aliwataka wananchi kuepuka kujenga mabondeni na  sehemu za njia za vianzio vya maji jambo ambalo litawasababisha maafa .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.