Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mhe. Ummy Mwalim (aliyenyoosha mkono) akimwelekeza eneo la ukaguzi
wa afya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Florens Turuka alipowasili
leo nchini katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA).
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Florens Turuka akinawa mikono kwa dawa maalum
eneo la ukaguzi wa afya alipowasili nchini leo katika Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). Hiyo ni moja ya kujikinga na
virusi vya homa ya mapafu ya Corona iliyotokea nchini China.
Afisa
Afya Mkuu Mazingira, Onesmo Kitange (wsa pili kushoto) leo akizungumza na
Mhe Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto wakati alipotembelea Jengo la
Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA), kujionea udhibiti wa homa ya mafua inayosababishwa na virusi vya
Corona.
Eneo
maalum la kusimama abiria wanaowasili nchini wakitokea nchi mbalimbali kwa
ajili ya ukaguzi wa afya, endapo watagundulika na homa ya mapafu
inayosababishwa na virusi vya Corona, iliyoanzia nchini China.
Mtawa
Michaela Chaudrasekar kutoka nchini India,
akipimwa joto la mwili kwa kutumia kifaa maalum cha mkono na Afisa Afya
Mkuu Mazingira, Onesmo Kitange alipowasili nchini leo kwenye Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA, ili kutambua endapo
ameambukizwa virusi vya homa ya mapafu aina ya Corona vilivyoanzia nchini
China.
No comments:
Post a Comment