Habari za Punde

Uongozi wa CRDB Nchini Umeazimia Kuunga Mkono Utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ya Maendeleo Kwa Wananchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bwana Abdulmajid Mussa Nsekela Kushoto akisisitiza msimamo wa Taasisi yake kushirikiana na Serikai katika kuendeleza Miradi ya Maendeleo inayowagusa Wananchi.

Na.Othman Khamis.OMPR. 
Uongozi wa Benki ya CRDB Nchini umeazimia kuunga mkono Utekelezaji wa miradi mbali mbali ya Maendeleo inayowagusa moja kwa Moja Wananchi kwa kushirikiana na Serikali katika kuona ustawi wa Jamii Mjini na Vijijini unaimarika kila siku.

Azma hiyo itabeba Sekta za Kilimo, Afya, Viwanda, Biashara Miundombinu ya Bara bara pamoja na Wajasiriamali kutokana na uzoefu mkubwa uliopelekea mafanikio makubwa ya ufanisi wa  Benki hiyo iliyoanzishwa mnamo Mwaka 1996 na kuorodheshwa katika soko la Hisa la Dar es salaam Mwezi Juni Mwaka 2009.

Akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ya CRDB Bwana Abdulmajid Mussa Nsekela  alisema Benki hiyo iliyopata Tuzo ya Mfuko wa Kimataifa wa Mazingira itadhihirisha Utekelezaji wa Fasafa yake  kwa kuendeleza dhamira ya kutoa huduma bora kwa Umma kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano {|TEHAMA}.
                                                                                                    Bwana Abdulmajid Mussa alisema  Taasisi hiyo ya Kifedha ya Kiafrika  inayoongoza   kutoa huduma za Kifedha Nchini Tanzania ambazo kwa sasa huduma hizo pia zikipatikana Nchini Burundi na Ukanda wa Afrika Mashariki imejipanga kufanya Kongamano kubwa Visiwani Zanzibar kwa kushirikiana na Wafanyabiashara na Wadau wengine.                                                                                          

Alisema mkusanyiko huo utakaokuwa mpana na huru zaidi kwa washiriki wake utalenga kuibua Miradi mbali mbali sambamba na kuweka Mikakati itakayosaidia kutanzua changamoto tofauti zilizopo Nchini ambazo huleta usumbufu katika uendelezaji wa Miradi iliyoanzishwa.

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Benki ya CRDB aliwapongeza Wananchi wa Zanzibar walioamua kupata huduma kupitia Taasisi hiyo ya Kifedha iliyopandisha hisa kwa Wateja wake iliyofikia Shilingi Bilioni 91 sawa na asilimia 95% hadi Mwaka 2018.
Bwana Aludmajid Mussa alimueleza Balozi Seif  kwamba Benki hiyo kwa sasa imefanikiwa kuongezeka kwa hisa yake ya asilimia 150% ikitarajiwa kupanda  zaidi kwa asilimia 250% bapo baadae.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliupongeza Uongozi wa Benki hiyo ya CRDB kwa sera zake zilizojikita kusaidia Wananchi hasa Sekta ya Ujasiri Amali.
Balozi Seif alisema inapendeza kuona Benki hiyo bado haijawahi kutetereka kama zilivyowahi kutokea baadhi ya Taasisi nyengine za Kifedha Nchini kutokana na kuongezeka kwa idadi ya Wanachama kila Mwaka.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba CRDB ni Benki inayowalenga moja kwa moja Wananchi walio wengi hasa wale wa Vijijini wanaojishughulisha zaidi na Sekta ya Kilimo ambayo ndio tegemezi kuu la Pato la Taifa.







No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.