Habari za Punde

Wajumbe wa TASAF Unguja Watakiwa Kusimamia Vyema Utekelezaji wa Miradi Mbalimbali Katika Maeneo Yao.Ili Kufanikisha Lengo la Serikali.

Mwenyekiti wa kamati ya usimamizi ya TASAF Unguja kutoka Tume ya mipango Dr. Ahmed Makame aliwakumbusha wajumbe hao kusimamia vyema utekelezaji wa miradi mbali mbali katika maeneo wanayofanyia kazi.
Mratibu wa TASAF Unguja Makame Ali Haji alieleza hayo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mpango wa kunusuru kaya maskini kwa wajumbe wa kamati ya usimamizi ya TASAF kwenye Ofisi za TASAF zilizopo Mazizini.
Mwenyekiti wa kamati ya usimamizi ya TASAF Unguja kutoka Tume ya mipango Dr. Ahmed Makame aliwakumbusha wajumbe hao kusimamia vyema utekelezaji wa miradi mbali mbali katika maeneo wanayofanyia kazi.
Afisa kutoka TASAF Ndugu Ibrahim Khalid Abdulla akiwasilisha taarifa ya muelekeo wa kupunguza kaya maskini kwa kipindi cha Pili kwa Wajumbe wa kamati ya usimamizi ya TASAF.
Wajumbe wa kamati ya usimamizi ya TASAF Wakichangia mada mbali mbali zilizowasilishwa kwao za utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mpango wa kunusuru kaya maskini.

Na.Kassim Salum.OMPR.
Zaidi ya Shillingi Bilioni tano zimetumika katika kutoa ajira kwa walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini kwa utekelezaji wa miradi 325 kupitia sekta za mazingira, misitu,bara bara, maji, uvuvi na kilimo kwa upande wa kisiwa cha Unguja.

Mratibu wa TASAF Unguja Makame Ali Haji alieleza hayo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mpango wa kunusuru kaya maskini kwa wajumbe wa kamati ya usimamizi ya TASAF  kikao kilichofanyika katika Ofisi za TASAF zilizopo Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Mratibu Makame alisema kupitia mpango wa kuweka akiba na kukuza uchumi wa kaya vikundi 1,147 vyenye jumla ya walengwa 15,968 ikiwa wanawake 15,354 na wanaume 614 vimeundwa kutoka shehia 126 za Unguja na kupatiwa mafunzo mbali mbali yanayohusiana na kuweka akiba na kukuza uchumi.

Alifafanua kuwa utekelezaji huo wa miradi imewezesha kukamilishwa kwa ujenzi wa huduma za miundombinu ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya cha Kianga kilichosaidia kuwapunguzia wananchi masafa kwa kutoa huduma bora sambamba na kukamilika kwa ujenzi ya nyumba ya daktari  iliyopo Kijiji cha Kijini Matemwe iliyogharimu jumla ya shilling milioni 247,385,964/-.

Alisema ujio wa Mpango wa kunusuru kaya maskini umewezesha wanawake wengi kuimarika kimaisha kwa kujiingizia kipato hali iliopelekea kustawika kwa familia ikilinganishwa na kipindi ambacho kabla ya ujuio wa mpango huo.

Mratibu Makame alifahamisha miongoni mwa faida zilizopatikana katika utekelezaji wa mpango wa awamu ya kwanza ni pamoja na kuimarika kwa umoja na ushirkiano kwa wanajamii wenyewe, kukua kwa matumizi ya teknolojia kama vile mitandao ya simu husuani kwa wananchi wanaoishi vijijini pamoja na wananchi waliowengi kujihusisha na kilimo cha mboga mboga chenye tija kubwa na kwa muda mfupi.

Alisema  hata hivyo  zipo baadhi ya changamoto zilizoukabili mpango huo ikiwemo kuhama kwa walengwa kwenda shehia nyengine hasa kwa mkoa wa Mjini Magharibi, kutopita kwa maafisa ugani kwa walengwa kwa ajili ya kuwakagua na kutatua changamoto za maradhi yanawaikumba sekta ya kilimo na mifugo.

Wakichangia mada washiriki wa kikao hicho walisema kutokana na mafanikio mazuri yaliyopatikana katika mpango wa kunusuru kaya maskini kuna haja ya kuwepo na usimamizi mzuri wa walengwa ili waweze kuzalisha bidhaa zenye thamani itakayosaidia kupatikana kwa soko rahisi kwa bidhaa zao.

Pamoja na mambo mengine washiriki hao walishauri  kwamba  ushirikiano baina ya sekta na sekta unahitajika katika kutatua changamoto zinazowakabili walengwa kutoka kaya maskini na kuacha tabia iliozoeleka kwa watendaji wa sekta kuwapitia watu wenye uwezo pekee.

Kwa Upande wake Afisa kutoka TASAF Ndugu Ibrahim Khalid Abdulla akiwasilisha taarifa ya muelekeo wa kupunguza kaya maskini kwa kipindi cha Pili alisema miradi ya kutoa ajira za muda ndio itakayopewa kipaumbele zaidi katika mpango huo ili kuwaongezea kipato walengwa pamoja na kuwawezesha kupata ujuzi.

Ndugu Ibrahimu alieleza kuwa mpango pia utaangalia zaidi watu wenye mahitaji maalum, watoto wenye mazingira magumu pamoja na wazee wanaoishi katika hali ngumu kwa kuwapatia ruzuku hata ikiwa hawana shughuli mahususi ya kujishughulisha nayo.

Alieleza mradi wa kipindi cha pili utawashirikisha kikamilifu wadau katika hatua tofauti za utekelezaji wa mpango ili kuufanya uwe na nguvu zaidiWna kujengea usimamizi madhubuti utakaosaidia kupunguza hali ya umaskini.

Akifunga kikao hicho cha siku moja Mwenyekiti wa kamati ya usimamizi ya TASAF Unguja kutoka Tume ya mipango Dr. Ahmed Makame aliwataka wajumbe hao kusimamia vyema utekelezaji wa miradi mbali mbali katika maeneo yao ili kufanikisha lengo la serikali la kuwapatia huduma bora wananchi wake ikiwemo kupunguza hali ya umaskini Nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.