Habari za Punde

ZAPAO na LSF Yaviwezesha Vikundi vya Vijana Kiuchumi Kuendesha Biashara

Na. Takdir Suweid Maelezo Zanzibar.
Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wasaidizi wa Sheria Zanzibar (ZAPAO) Ndg.Nassor Muhammed amewashauri Wafanyabiashara wadogo wadogo kufuata Miongozozo na Kanuni za Biashara zilizowekwa na Serikali ili kuepuka Migogoro kati yao.
Akizungumza kwa niaba yake katika Ukumbi wa Hospitali ya Wagonjwa wa Akili Kidongochekundu Wilaya ya Mji kwa wafanyabiashara wadogo wa Wilaya 3 za Mkoa wa Mjini Magharibi Ndg. Issa Mwinchoum Suleiman kutoka ZAPAO amesema baadhi yao wanafanya biashara bila ya kuwa na Leseni,Kulipa kodi na kuuza sehemu zisizoruhusiwa jambo ambalo linasababishia hasara katika biashara zao.
Hivyo mafunzo hayo yataweza kupata uelewa wa kuendesha biashara kwa kufuata Sheria na  kuepuka hasara.
Aidha amesema kundi kubwa la Vijana na akinamama ambao hawana ajira hivyo ZAPAO kwa kushirikiana na LSF wameandaa kuwawezesha kiuchumi ili kuyawezesha makundi hayo kupata ajira na kuendesha familia zao.
Hata hivyo amewakumbusha Wafanyabiashara hayo kuyafanyia kazi mafunzo wanayopewa na Taasisi za Serikali na Binafsi ili kuweza kuleta mabadiliko ya kuendesha bidhaa zao.
 Kwa upande wake Makamo Mwenyekiti wa ZAPAO Sabahi Bakari Hassan amesema wamefanya utafiti na kubaini baadhi ya Wafanyabiashara wanakinzana na Sheria jambo ambalo linaweza kuwasababishia kushindwa kufanyabiashara na kufikia malengo waliokusudia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.