Habari za Punde

ZIARA YA MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) MKOANI DAR ES SALAAM KUKAGUA VITUO VYA KUANDIKISHA WAPIGA KURA

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Rufaa (Mst.) Semistocles Kaijage (aliyevaa kofia) akisikiliza maelezo ya Afisa Tehama wa Tume, Ndugu. Sanif Khalifan (kulia) leo (tarehe 15.02.2020) alipotembelea kituo cha kuandikisha wapiga kura kilichopo kwenye Viwanja vya Leaders, Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Jaji Kaijage yupo kwenye ziara ya kukagua vituo vya kuandikisha wapiga kura kwenye zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambalo limeanza tarehe 14.02.2020 Kwenye Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku saba (7) mfululizo ambapo vituo vitafunguliwa saa 02:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni. 
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Rufaa (Mst.) Semistocles Kaijage akisaini kitabu cha wageni leo (tarehe 15.02.2020) katika kituo cha kuandikishia wapiga kura kilichopo Hospital ya Taifa ya Muhimbili, Kata ya Upanga Magharibi, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Jijini Dar es Salaam.  Jaji Kaijage yupo kwenye ziara ya kukagua vituo vya kuandikisha wapiga kura kwenye zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambalo limeanza tarehe 14.02.2020 kwenye Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku saba (7) mfululizo ambapo vituo vitafunguliwa saa 02:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Rufaa (Mst.) Semistocles Kaijage akisaini kitabu cha wageni leo (tarehe 15.02.2020) akisikiliza maelezo ya Afisa Tehama wa Tume, Bi. Fina Kidunda alipotembelea kituo cha kuandikisha wapiga kura cha Hospital ya Taifa ya Muhimbili, Kata ya Upanga Magharibi, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Jijini Dar es Salaam.  Jaji Kaijage yupo kwenye ziara ya kukagua vituo vya kuandikisha wapiga kura kwenye zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambalo limeanza tarehe 14.02.2020 kwenye Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku saba (7) mfululizo ambapo vituo vitafunguliwa saa 02:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

(PICHA ZOTE: IDARA YA HABARI NA ELIMU YA MPIGA KURA-NEC)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.