Habari za Punde

Jumuiya ya Maimamu Jijini Zanzibar Yatoa Tamko Kuhusu Maradhi ya Corona.

Na Kijakazi Abdalla - Maelezo Zanzibar, 19/03/2020
Maimamu wa Misikiti wametakiwa kufanya maombi (Istighfara) maalum kila kipindi cha  swala ili kumuomba Mwenyezi Mungu atuondoshee  maradhi ya Corona.
Hayo ameyasema Naibu Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) Khamis Yussuf Khamis wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na  mripuko wa maradhi ya Corona.
Amesema  maradhi ya corona yamekuwa ni janga duniani ,hivyo hakuna budi kumuomba Mwenyezi Mungu  ili aweze kutuondoshea maradhi hayo kila kipindi cha swala.
Aidha amewataka maimau kufupisha hotuba za swala ya Ijumaa   na kutoa zenye kufahamika ili kuondosha mkusanyiko  kuwa wa muda mrefu kwa kipindi hichi kilichojitokeza kwa maradhi ya corona.
Vilevile amewaka wazazi kuchukua juhudi za kuwasomesha watoto masomo ya chuoni na skuli kwa kipindi hichi na kutowaacha kwa kipindi kirefu kushughulikia michezo.
“Nawasihi wazazi kuchukua jitihada kuhakikisha watoto wetu wanasoma masomo ya Skuli pamoja na chuoni na kutowacha kushughulikia mpira na kutizama TV”Alisisitiza Naibu Katibu Mtendaji huyo.
Hata hivyo amewaomba wazazi ambao  tayari wameshajiandaa kwa harusi kutozivunja bali wafuate masharti yaliyowekwa na Serikali ili kuhakikisha ndoa hizo zinafanyika kwa utaratibu uliowekwa.
Aidha amezitaka  Taasisi ambazo zinasafirisha Mahujaji kutoa  mafunzo ya hija  kwa njia za Cd pamoja kufungwa kwa chuo cha wale ambao waliokuwa wanajiataanda kwa mafunzo ya ndoa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.