Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher
Kadio, akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,
Ulinzi na Usalama, kabla ya Kamati hiyo kupokea taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa
Kiwanda cha Useremala cha Magereza, Msalato Mkoani Dodoma, leo. Wajumbe hayo
walitoa ushauri wa kuboresha ujenzi wa Kiwanda hicho ambao tayari umenza.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya
Nje, Ulinzi na Usalama, Salim Mwinyi Rehani, akizungumza katika kikao cha
Kamati hiyo kilichojadili Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Useremala cha
Magereza, Msalato Mkoani Dodoma, leo. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio. Kushoto ni Katibu wa Kamati hiyo,
Ramadhani Abdalla, na kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Suleiman
Mzee.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher
Kadio (kulia), akisalimana na Katibu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya
Nje, Ulinzi na Usalama, Ramadhani Abdalla, wakati alipokuwa anawasili na
Wajumbe wa Kamati hiyo kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa
Kiwanda cha Useremala cha Magereza, Msalato Mkoani Dodoma, leo
Mhandisi wa Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Useremala cha
Magereza, Bonaza Malata (kulia), akiwaonyesha Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Ujenzi wa Kiwanda hicho kilichopo
Msalato Mkoani Dodoma, leo. Kamati hiyo ilipokea taarifa ya Mradi huo ambao
tayari umeanza na kutoa ushauri wa kitaalamu wa ujenzi wa Kiwanda hicho. Wapili
kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Salum Mwinyi Rehani, na watatu kulia
ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio.
Mhandisi wa Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Useremala cha
Magereza, Bonaza Malata (kulia), akiwafafanulia jambo Wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kuhusu Ujenzi wa Kiwanda hicho
kilichopo Msalato Mkoani Dodoma. Kamati hiyo ilipokea taarifa ya Mradi huo
ambao tayari umeanza na pia kutoa ushauri wa kitaalamu wa ujenzi wa Kiwanda
hicho. Watatu kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Salim Mwinyi Rehani,
na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher
Kadio.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment