Habari za Punde

Mawaziri SMT na SMZ wataka Sekta ya Habari ikuze Kiswahili

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Tanzania Dk Harrison Mwakyembe akichangia mada kuhusiana na Taarifa ya Kikao cha Kwanza cha Tarehe 4 mach mwaka 2020 cha Mawaziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezi(SMT)Habari Utalii na Mambo ya Kale (SMZ) na Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo katika ukumbi wa ZSSF Kariakoo Zanzibar.
Waheshimiwa Mawaziri wakitiliana saini Ushirikiano wa Kiutendaji katika mambo yasiousiana na Muungano katika hafla iliofanyika ukumbi wa ZSSF Kariakoo Zanzibar. wamwanzo kushoto ni  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Tanzania Dk Harrison Mwakyembe (SMT),Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale (ZNZ)Mahmoud Thabit Kombo katikati na Waziri wa  Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Baloz Ali Karume.
Naibu Waziri wa Habari Utalii  na Mambo ya Kale Chumu Kombo Khamis  akichangia mada kuhusiana na Taarifa ya Kikao cha Kwanza cha Tarehe 4 mach mwaka 2020 cha Mawaziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezi(SMT)Habari Utalii na Mambo ya Kale (SMZ) na Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo katika ukumbi wa ZSSF Kariakoo Zanzibar.
Naibu Waziri Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Lulu Msham Abdalla akichangia mada  kuhusiana na Taarifa ya Kikao cha Kwanza cha Tarehe 4 mach mwaka 2020 cha Mawaziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezi(SMT)Habari Utalii na Mambo ya Kale (SMZ) na Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo katika ukumbi wa ZSSF Kariakoo Zanzibar.
Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA)Mwanahija Ali Juma kichangia mada  kuhusiana na Taarifa ya Kikao cha Kwanza cha Tarehe 4 mach mwaka 2020 cha Mawaziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezi(SMT)Habari Utalii na Mambo ya Kale (SMZ) na Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo katika ukumbi wa ZSSF Kariakoo Zanzibar. 

Na Issa Mzee Maelezo Zanzibar. 5/3/2020
Serekali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na Serekali ya Muungano Tanzania inaendelea kutatua changamoto zilizomo katika muungano kwenye sekta ya habari  ili kukuza lugha ya Kiswahili nchini.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mhe, Mahamoud Thabit Kombo katika Ukumbi wa ZSSF Kariakoo katika ghafla ya utiaji saini kuhusu Ushirikiano wa Utendaji wa mambo yasiyo ya Muungano katika Wizara zenye dhamana ya mambo ya habari.
Amesema makubaliano hayo yatasaidia katika matumizi ya ndege zisizo na rubani na upatikanaji wa chanali ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) katika ving’amuzi vyote nchini bila ya malipo kwa lengo la kuimarisha uhusiano na kukuza lugha ya hiyo Nchini.
Amefahamisha kuwa makubaliano hayo pia yataendeleza ukuaji wa Kiswahili kimataifa kwa kutoa waandishi wa habari kutoka Tanzania amabao watatumia na kukitangaza Kiswahili katika vyombo hivyo pamoja na uanzishwaji wa vituo vya utamaduni nje ya nchi.
Waziri Kombo ameeleza kuwa wataendeleza kutangaza utalii na utamaduni nje ya nchi na kuimarisha michezo pamoja na kukuza utendaji kwa lengo la kuleta maendeleo nchini.
Aidha Waziri Mahamoud amefahamisha kuwa jukumu la kufundisha na lugha ya Kiswahili nchini ni Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) na baraza la Kiswahili la Tanzania (BAKITA) hivyo ni vyema kutoa wataalamu wazuri wataofundisha lugha hiyo ili iweze kukua na kuimarika zaidi.
“Inashangaza sana kumkuta mtu asie Mtanazania anafundisha Kiswahili nje ya nchi au waajiriwa wasio Watanzania wanaajiriwa kwa kigezo cha lugha ya Kiswahili,mfano wa wazi ni shirika l ndege la kimataifa la Emirates Airline waajiriwa wengi walioajiriwa kwa minajili ya kutumia Kiswahili ni Wakenya na sio Watanzani ni jambo la kushangaza” alisema Waziri Mahamoud.
Kwa upande wake Waziri wa habari wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazania Dkt Harrison Mwakyembe amesikitishwa na baadhi ya raia wasio Watanzania kutumia njia hiyo ya kutumia lugha ya kiswahili ili kupata ajira bila ya watanzania wenyewe kufaidika nayo .
Nae Waziri wa Vijana Sanaa Utamaduni na Michezo  Balozi Ali Karume alisema mashirikano hayo yana umuhimu mkubwa kwani yatapelekea kubadilishana na kupanua wigo katika kuleta maendeleo katika sekta ya habari na Utamaduni  lengo la kuimarisha utendaji.
Balozi Ali Karume amefahamisha kuwa katika mambo ya michezo ni lazima kushirikiana kwa pamoja katika kufanya shughuli zao  ikiwemo Kombe la M apinduzi ili kukuza lugha ya Kiswahili wakati watakapokwenda kufanya mashindano nje ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.