Habari za Punde

Meneja wa ZECO Azungumza na Waandishi wa Habari Zanzibar Kuhusiana na Tatizo la Umeme Mdogo Baadhi ya Maeneo.

Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Hassan Ali Mbarouk akizungumza na Waandishi wa Habari Kuhusu Utendaji Kazi katika Shirika hilo Huko Ofisini kwake Gulioni Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa habari Wakimsikiliza Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Hassan Ali Mbarouk kuhusu Utendaji wa Kazi katika Shirika hilo hafla iliyofanyika Ofisini kwake Gulioni Mjini Zanzibar.
Picha Na Maryam  Kidiko – Maelezo Zanzibar.

Na Issa Mzee Maelezo Zanzibar      12/03/2020.
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Hassan Ali Mbarouk amesema kuwepo kwa tatizo la umeme mdogo katika baadhi ya maeneo ya mji wa Zanzibar yanatokana na ongezeko la watumiaji pamoja na ujenzi holela.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake huko Gulioni Mjini Unguja kuhusiana na mafanikio na changamoto zinazoikabili shirika hilo.
Amesema Shirika hilo linachukua jitihada ya kufunga mashine kubwa (transfoma) katika maeneo hayo ili kuweza kukidhi mahitaji ya matumizi na kuondosha usumbufu kwa wananchi.
Meneja huyo amefahamisha kuwa shirika hilo linakabiliwa na changamoto ya wizi wa mita, umeme, baadhi wananchi na mashirika kutolipa madeni kwa wakati na utapeli unaofanywa na baadhi watu kujifanya watumishi wa shirika hilo kwa lengo la kuiba na kupelekea kulitia hasara shirika.
“Licha ya kuwa shirika linachukua jitihada za hukakikisha kuwa upatikanaji wa huduma ya umeme mijini na vijijini upo vizuri lakini bado tunakabiliwa na changamoto ya wizi wa mita, umeme, baadhi ya wananchi na mashirika kutolipa madeni yao kwa wakat, na matapeli wanaolaghai wananchi kwa kujifanya watumishi wa shirika kwa lengo la kuibia wananchi jambo ambalo hukosesha mapato ya shirika”.
Aidha ameeleza kuwa matumizi ya umeme yamepanda kwa kasi  Zanzibar kutoka mega watt 40 mwaka 2008 na kufikia mega watt 70 mpaka 90 mwaka huu ambapo shirika hilo lina uwezo wa kuzalisha mega watt 140 kwa siku
Akizungumzia mafanikio Meneja huyo amesema shirika hilo  limefanikiwa Meneja huyo alisema shirika hilo limeweza kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kufikisha umeme vijijini na katika visiwa vidogo  vya Unguja na Pemba.
“Katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi  shirika limeweza  kufikisha umeme vijijini na katika visiwa vidogo  vya Unguja na Pemba, ambapo vijiji 520 vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo nane kati ya kumi vilivyotakiwa kupata umeme tayari visiwa nane vinapata nishati hiyo”, ameeleza Meneja huyo.
Akitoa ufafanuzi kuhusu deni la bilioni 65 linalodaiwa shirika la umeme la Zanzibar  na shirika umeme Tanzania Bara (TANESCO) amesema kuwa tayari fedha zimeshalipwa  ambapo zimebaki bilioni 10.7 kumalizia deni hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.