Habari za Punde

Naibu Waziri Shonza:Wizara ipo tayari kumpa ushirikiano Chidbenz


Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo mheshimiwa Juliana Shonza akimsisitiza msanii wa bongofleva Rashid Abdallah maarufu kama Chid benz kufanya kazi kwa bidii na kuwa mbunifu huku akimhakikishia kuwa serikali ipo tayari kumpa ushirikiano alipokuwa akifanya kikao nae leo jijini Dodoma.


Msanii wa bongofleva nchini Rashid Abdallah maarufu kama Chid benz akimweleza Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo mheshimiwa Juliana Shonza (kulia) kuwa mapema wiki ijayo anatarajia kutoa video ya wimbo wake wa Beautiful na pia atatunga wimbo wa kuhusu Corona katika kikao kilichofanyika leo jijini Dodoma.


Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo mheshimiwa Juliana Shonza akiwa akimsisitiza msanii wa bongofleva Rashid Abdallah maarufu kama Chid benz kuwa wizara ipo tayari kumpa ushirikiano wakati wowote na kikubwa ni msanii huyo kujituma na kuonyesha umma kweli ameachana na matumizi ya madawa ya kulevya mara baada ya kikao leo jijini Dodoma.Na Anitha Jonas – WHUSM Dodoma.
Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amwaahidi ushirikiano msanii wa bongofleva nchini Rashid Abdallah maarufu Chidbenz.

Mheshimiwa Shonza ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma alipofanya kikao na msanii huyo ambapo Chid benz alimuhakikishia kuwa kwa sasa  amebadilika na anataka kuwaonyesha watanzania amefanikiwa kujikwamua katika matumizi ya madawa ya kulevya na hataki tena kurudi huko kwani anazaidi ya miezi mitatu sasa hajatumia madawa hayo kabisa.

“Kati ya wasanii wenye kukubalika  na mashabiki zao wewe Chid benz  ni mmoja wao na mashabiki zako ni wengi hivyo ningependa kukuona kwanzia sasa unalijenga zaidi  jina lako kwa kuonyesha kuwa umebadilika,katika kipindi hichi nitafurahi zaidi kukuona unasonga mbele na hurudi tena katika matumizi ya madawa ya kulevya wizara ipo pamoja  na wewe kukusaidia wakati wowote ,”alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika  kikao hicho mheshimiwa Shonza alimsisitiza msanii huyo kuwaonyesha  watanzania kuwa anaweza na hata akipewa nafasi anaweza kujitumia vyema  na kuonyesha juhudi yake katika kufanya kazi na kuwa mbunifu katika kufanya kazi zake za usanii.

Naye Msanii huyo wa Bongofleva Chid benz alieleza kuwa kwa sasa hautarudi nyuma tena sababu tayari amekwisha acha kutumia  matumizi ya madawa hayo na ninaelewa bahati haiji mara mbili lakini kwangu naiona imekuja zaidi ya mara moja kwa maana ya kuwa nimekuwa nimekuwa na anguka nainuka narudi kwa mashabiki wananipokea nakuendelea kukubali muziki wangu hakika najiona niwakati wa kuwafurahisha zaidi mashabiki na sitawaangusha.

“Ombi langu kwa serikali ni kupata ushirikiano na mapema wiki ijayo ninatarajia kutoa wimbo wangu mmoja uitwao Beautiful ambao nimeuiamba nikisifu uzuri wa mwanamke na kufuatia janga la Corona ninamwahidi mheshimiwa Naibu Waziri kuwa nitatunga wimbo kwa ajili ya Corona ,”Chid benz.

Pamoja na hayo nae Chid benz alitoa wito kwa watanzania kuacha kufanya mzaha katika mitandao ya jamii kuhusu suala la ugongwa Corona sababu hili ni tatizo ni janga linalosumbua dunia kwa sasa hivyo jambo la msingi ni kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na serikali kutoka kwa wataalamu wa afya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.