Habari za Punde

WATUMISHI MADINI WAPATA ELIMU CORONA

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Issa Nchasi akiwakaribisha wataalamu wa Afya kutoa mafunzo juu ya ugonjwa wa corona kwa watumishi wa Wizara ya Madini Makao Makuu jijini Dodoma, leo asubuhi.

Na.Asteria Muhozya na Nuru Mwasampeta - Dodoma 

Watumishi wa Wizara ya Madini wakiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Issa Nchasi leo Aprili 2, wametembelewa na wataalamu wa afya kwa lengo la kutoa elimu juu ya ugonjwa wa corona unaosababishwa na virusi vya covid-19 na namna ya kujikinga na ugonjwa huo. 

Wataalamu hao ni pamoja na Dkt. Shamza Said ambaye ni miongoni mwa wataalamu wa afya wanaojishughulisha na magonjwa yanayoambukiza kwa kasi aliyeambatana na Toyi Veronica mtaalamu wa mazingira katika masuala ya afya. 

Akizungumzia virusi vinavyosababisha ugonjwa huo Dkt. Shamza alisema virusi vya covid-19 ni virusi vipya kuwepo duniani vya aina hiyo vinavyotoka kwa wanyama na kusababisha madhara kwa binadamu. 

Amesema virusi hivi pindi vinapoingia mwilini mwa binadamu vinasababisha madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushambulia mfumo wa upumuaji, figo, ini na madhara mengine na kuwasihi watumishi na jamii pindi wanapohisi kuwa na dalili za ugonjwa huo, kuhakikisha wanawahi katika vituo vya afya ili kupatiwa huduma stahiki kabla ya ugonjwa kusababisha madhara makubwa mwilini. 

Amesema, unapowahi kupata huduma za kitabibu kuna uwezekano mkubwa wa kupona tofauti na mtu anayekwenda kutibiwa awapo katika hali mbaya. 

Aidha, Dkt Shamza amewashauri watumishi kupunguza mikusanyiko isiyokuwa ya lazima, kunawa kwa sabuni na vitakasa mikono kila wakati, kuacha kukusanyika katika masherehe, matumizi ya vifaa vya vyakula yasiwe shirikishi, kuzingatia uvaaji sahihi wa mask pamoja na kuwa wawazi wanapojihisi kuwa na maambukizi ya ugonjwa ili kuepusha kuambukiza watu wengine. 

Kwa kuhitimisha, Dkt. Shamza amewataka watumishi kutoa elimu ya corona kwa watu wengine katika familia ndugu jamaa na marafiki ili elimu hii iwafikie wengi na waweze kujikinga na hivyo kupunguza maambukizi nchini. “Unapopata elimu, elimisha na wengine” amisisitiza Dkt. Shamza. 

Kwa kuhitimisha, Dkt. Shamza amewataka watumishi kutoa elimu ya corona kwa watu wengine katika familia ndugu jamaa na marafiki ili elimu hii iwafikie wengi na waweze kujikinga na hivyo kupunguza maambukizi nchini. “Unapopata elimu, elimisha na wengine” alisisitiza. 

Kwa upande wake, Mtaalamu wa mazingira katika masula ya Afya, Koyi Veronika ameushauri uongozi wa wizara kupunguza vikao kazi vya ana kwa ana na badala yake uongozi kwa kushirikiana na wataalamu wa TEHAMA kuratibu mfumo wa kutumia mtandao katika vikao vyao ili kuepusha maambukizo miongoni watumishi. 

Kwa kuhitimisha, Dkt. Shamza amewataka watumishi kutoa elimu ya corona kwa watu wengine katika familia ndugu jamaa na marafiki ili elimu hii iwafikie wengi na waweze kujikinga na hivyo kupunguza maambukizi nchini. “Unapopata elimu, elimisha na wengine” alisisitiza. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala, Issa Nchasi amewashukuru Wizara ya Afya kwa mpango mzuri walioanzisha wa kupita na kutoa elimu kwa watumishi na kuahidi kuyasimamia yote waliyoelekeza ili kupambambana na gojwa hatarishi la corona. 

Baada ya kutoa elimu hiyo zilipo ofisi zaWizara Makao Makuu, wataalamu hao wameelekea zilipo ofisi za Taasisi ya Jiolojia na Utafiti na Ofisi ndogo za Wizara ya Madini, Chuo cha Madini na kumalizia mafunzo hayo ofisi za Tume ya Madini. 

Mtaalamu wa afya Dkt. Shamza Said akitoa elimu ya ugonjwa wa corona kwa watumishi wa Wizara ya Madini ili kuwapa uelewa wa ugonjwa huo na namna ya kujikinga
Mtaalamu wa afya Dkt. Shamza Said akitoa elimu ya ugonjwa wa corona kwa watumishi wa Wizara ya Madini ili kuwapa uelewa wa ugonjwa huo na namna ya kujikinga.

Watumishi wa Wizara wakifuatilia mafunzo juu ya ugonjwa wa corona kutoka kwa wataalamu wa afya (hawapo pichani)
Mtaalamu wa mazingira katika masula ya Afya, Koyi Veronika akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo yaliyotolewa kwa watumishi ofisi za Wizara ya Madini Makao Makuu, jijini Dodoma
Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi, Veneranda Charles akiuliza swali kwa wataalamu wa afya juu ya vitakasa mikono vinavyoshauriwa kutumika ili kujikinga na ugonjwa wa corona.

Kamishna msaidizi wa Madini anayeshughulikia masuala ya Ushiriki wa wananchi na ncchi katika uchumi wa madini, Ngole akiuliza swali kwa wataalamu wa afya mafunzo hayo yakiendelea.
Dkt. Shamza Said akijibu maswali juu ya ugonjwa wa Corona aliyoulizwa na watumishi.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala, Issa Nchasi, akiwashukuru na kuwaaga wataalamu wa Afya mara baada ya zoezi la kutoa mafunzo juu ya ugonjwa wa corona kwa watumishi wa Wizara ya Madini Makao Makuu, kukamilika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.