Habari za Punde

Wazazi tusiwatume watoto kwenye sehemu za mikusanyiko kama masokoni


Mbali ya Serikali kuzifunga Skuli na Madrasa ili watoto watulie nyumbani ili kujilinda na maambukizi ya maradhi ya Corona, baadhi ya wazee wamekuwa na tabia ya kuwatuma watoto hao sokoni jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.

Leo tarehe 2/4/2020 Dawati Mkoa wa Mjini Magharibi kwa kushirikiana na uongozi wa Soko la Mbogamboga la Mombasa na Halmashauri ya Wilaya ya Magharib B, walikuwepo sokoni hapo na kufanikiwa kuwazuia watoto 16 ambao ni miongoni mwa watoto waliokwenda sokoni hapo.

Baada ya kuzuiliwa, watoto hao walipelekwa Dawati la kituo cha Polisi cha Mazizini ambapo wazee wa watoto hao pamoja na watoto walifahamishwa umuhimu wa watoto hao kubakia nyumbani hasa kwa kipindi hichi.

Wazazi tunaombwa kuchukua kila aina ya tahadhari kujikinga na kujiepusha na maradhi ya Corona kwani watoto ndio wabebaji wakubwa (Vectors) ambao wanaweza kuiathiri familia nzima nyumbani kwa kuiambukiza ilhali wao wakiwa na  nafasi ndogo ya kuugua kutokana na kuwa na kinga nzuri mwilini mwao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.