Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Apokea Misaada Kwa Ajili ya Mapambano Dhidi ya Ugonjwa wa CORONA COVID -19.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya  sh. 4, 000,000,000/= kutoka kwa Meneja Mkazi  (Country Manager) wa Kampuni ya Madini ya Barric - Twiga Minerals, Hilaire Diarra (kushoto) na Msaidizi wake, Neema Ndossi (kulia)  ukiwa ni mchango wa Kampuni hiyo kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 8, 2020. Wa pili kushoto ni Waziri wa madini, Doto Biteko na wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea mchango wa  vifaa vya kuendeshea mikutano kwa njia ya video ambavyo ni cloudlink camera tatu, Cloudlink Mic tatu, Cloudlink TV terminal tatu, Cloudlink Platform pamoja na Thermal Imaging Temperature Measuring System moja vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 940 Kutoka campani ya TEHAMA ya HUAWEI,kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu - COVID-19. Pichani, Waziri Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Zhou Xu (wa tano kulia), Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Wu tao  (kushoto) na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, George Mwakyembe. Wa nne kulia  ni Waziri wa Madini, Doto Biteko, wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea lita 50,000 za mafuta kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya mafuta ya Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah ( wa pili Kushoto) na  Meneja Uzalishaji wa kampuni hiyo, Lameck Hiliyai (kulia) ukiwa ni mchango wa Kampuni hiyo wa kuunga mono mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID -19 nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 8, 2020. Wa tatu Kushoto ni Waziri wa Madini, Doto Biteko, Wa pili Kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, ofisi ya Waziri Mkuu, Kanalı Said Matamwe
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea mchango wa sh. 100, 000,000/= Kutoka kampuni ya Taifa Gas kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu - COVID-19. Pichani, Waziri Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Makampuni ya Taifa, Abdulkarim Shah (kulia) 
na Mkurugenzi Mtendaji wa Taifa Gas, Hamisi Ramadhani. Wa tatu kushoto ni Waziri wa Madini, Doto Biteko, wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanalı Said Matemwe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya sh. 1,000,000,000/= kutoka kwa Mfanyabiashara, Rostam Aziz (wa tatu kushoto)  ukiwa ni mchango binafsi wa mfanyabiashara huyo  wa kuunga mkono mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19.   Makabidhiano hayo yalifanyika  kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 8, 2020.  Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile,kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Makampuni ya Taifa, Abdulkarim Shah, wa pili ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Taifa Gas, Khamis Ramadhani na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Said Matamwe
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Sh. 79,000,000/=  ukiwa ni mchango wa ASASI za Kiraia wa kuunga mkono mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID-19 nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 8, 2020. Pichani Kutoka kushoto ni Edward Mbogo, Mkurugenzi wa Idara ya Maafa , Ofisi ya Waziri Mkuu,Kanali  Said Matemwe, Dkt. Stigmata Tenga, Lulu Ngw'anakilala, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile, Tike Mwambipile, Nasim Losai na kulia ni Brian Mosala.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  wadau mbalimbali waliojitokeza kutoa michango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za serkali za kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19 kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 8, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.