Habari za Punde

Misa Tanzania yaahidi kuendelea kupigania uhuru wa maoni



 Washiriki wa mkutano wa siku moja (1) ulioandaliwa na MISA-Tan uliojadili, pamoja na mambo mengine ,umuhimu na changamoto  za uhuru wa kujieleza na kupata taarifa nchini Tanzania.
Mshiriki Bw. Joseph Kavishe kutoka mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA)  akichangia mjadala kuhusu makosa ya mtandao na sheria zake wakati wa kikao cha majadiliano kilicho andaliwa na MISA-Tan.

Haji Mtumwa, Zanzibar

Imeelezwa kuwa tokea kuanzishwa kwake Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-Tan) imekua ikipigania uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa vyombo vya Habari.

Hayo yamebainika katika mkutano wa siku moja ulioandaliwa na MISA-Tan  uliojadili umuhimu na changamoto  za uhuru wa kujieleza na kupata taarifa nchini Tanzania, mkutano ambao umeongozwa na Mjumbe wa Bodi ya MISA-Tan, Michael Gwimile.

Moja wapo ya changamoto ilielezwa katika mkutano huo ni  uhuru wa kutoa maoni na kupata taarifa ni uwepo wa sheria mbalimbali, sheria hizo ni pamoja na sheria ya huduma za vyombo vya Habari, sheria ya makosa ya mtandao na sheria ya takwimu.

Kwa bahati mbaya waandishi wa Habari na wananchi kwa ujumla wana uelewa mdogo juu ya sheria hizi, mfano mzuri kumekuwa na ongezeko la makosa yatokanayo na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na hivyo kupelekea kuvunja sheria ya makosa ya mtandao.

Baadhi ya wahanga ni mwandishi wa Habari wa gazeti la Tanzania Daima tokea Zanzibar Bw. Talib ussi Hamad, aliesimamishwa kufanya shughuli za uandishi wa Habari kwa muda wa miezi sita baada ya kutoa taarifa kwenye ukurasa wake wa facebook akimtangaza mwandishi mwenzake kuwa ana corona.

Changamoto za uhuru wa kujieleza na kupata taarifa zimepelekea MISA-Tan kuandaa mkutano wa wadau mbalimbali wa vyombo vya Habari ili kujadili namna bora ya kuongeza uelewa juu ya namna sahihi ya kutumia mitandao ya kijamii.

Katika mkutano huo maswala kadhaa yalijadiliwa ikiwemo kutumia vyanzo sahihi vya taarifa na waandishi  na wananchi kujiridhisha na usahihi wa taarifa wanazopokea kabla ya kuzisambaza.













No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.