Habari za Punde

Wazazi WAtakiwa Kuwathibiti Watoto Wao Katika Eid Fitry Kujiepusha Maambukizo ya Corona.

Na.Takdir Suweid. Zanzibar.
Wazazi nchini wameshauriwa kuwadhibiti watoto wao kusherehekea Sikukuu ya Idil-fitri Majumbani mwao ili kujikinga na Maradhi ya Covid 19.
Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa Viti maalum Mwanaidi Kassim Mussa wakati alipokuwa akizungumzia Sikukuu ya Idil-fitri inayoendelea Kisiwanduwi Wilaya ya Mjini.
Amesema maradhi bado yapo licha ya kuwa yamepunguwa hivyo ni vyema Wazazi kufuata Misingi ya Wataalamu wa Afya ili kuwanusuru watoto na Mambukizi ya Virusi vya Corona.
Aidha amesema baadhi ya Wananchi wanakaidi maagizo yaliotolewa na Serikali hivyo ni vywma kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya Seria ili iwe fundisho kwao na wengine wenye nia ya kukiuka maagizo hayo.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Ofisi ya Zanzibar (UW) Tunu Juma Kondo amewashauri Wanawake kushirikiana na Viongozi wa Shehia kusimamia na kuhakikisha Watoto hawaweki mikusanyiko ya kwenda kucheza katika Viwanja ili kuwakinga na Janga la Corona na Udhalilishaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.