Habari za Punde

Mwanachama wa CCM Ajitokeza wa Kwanza Kuchukua Fomu ya Kugombewa Nafasi ya Urais wa Zanzibar Kupitia CCM

Katibu wa Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg. Casian Galos Nyimbo akimkabidhi fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar Mwanachama wa CCM Ndg. Mbwana Bakari Juma, akiwa ni mwanachama wa kwanza kufungua mlango kuwania kuteulewa na CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Rais wa Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Zoezi la kuchukua Fomu za Kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM umeaza leo hadi tarehe 30 mwezi huu. 
Mwanachama wa CCM Ndg. Mbwana Bakari Juma akiwa na kabrasha lake la Fomu ya Kugombea Urais kupitia CCM akiwa katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo.  
Katibu wa Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg. Galos Nyimbo akimpa maelezi jinsi ya ujazaji wa fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar  kupitia CCM Mwanachama wa CCM Ndg. Mbwana Bakari Juma, akiwa ni mwanachama wa kwanza kufungua mlango kuwania kuteulewa na CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Rais wa Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Mwanachama wa CCM Mgombea nafasi ya kuchaguliwa na Chama kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Ndsg. Mbwana Bakari Juma akipata maelezi ya jinsi ya ujazaji wa fomu hiyo kutoka kwa Maofisa wa CCM. 
Mgombea nafasi ya Urais kuteuliwa na CCM kugombea Urais wa Zanzibar Ndg. Mbwana Bakari Juma akizungumza na Waandishi wa habari Zanzibar sera yake endapo CCM itamteuwa kugombea nafasi hiyo adhma yake  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.