Habari za Punde

TANGA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI NA KIBIASHARA AMBAZO ZINAZOLETWA NA TPDCMkuu  wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katika akikata utepe leo kuashiria   uzinduzi wa kituo cha kuweka mafuta kinachoendeshwa na kampuni tanzu ya shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania ( Tan Oil.) kushoto ni   Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya  Petroli Tanzania (TPDC),Dk James Mataragio na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu uzinduzi huo ulifanyika kijiji cha Michungwani kata ya Segera wilayani Handeni  

Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya  Petroli Tanzania (TPDC),Dk James Mataragio akizungumza wakati wa uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa uzinduzi huo kulia ni Mkurugenzi   Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya  Petroli Tanzania (TPDC),Dk James Mataragio kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry ShekifuWANANCHI  wa Mkoa wa Tanga wametakiwa kuchangamkia fursa za kiuchumi na kibiashara ambazo zinaletwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) kupitia miradi yake katika sekta ya mafuta na gesi ambayo  inakuja mkoani humo. 

Hayo yamebaishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa  Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),Dk James Mataragio pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigela jana katika kijiji cha Michungwani kata ya Segera wilayani hapa katika hafla fupi ya uzinduzi wa kituo cha kuweka mafuta kinachoendeshwa na kampuni tanzu ya shirika hilo Tan Oil. 

Akizungumza katika hafla hiyo,Dk Mataragio amesema  kuwa shirika hilo limeingia rasmi katika mkakati wake wa kufufua biashara ya mafuta ambayo ilikuwepo tangu shirika hilo lilipoanzishwa mwaka 1969 kabla ya kusitisha huduma hizo.


Amesema  kuwa mkakati huo sio lengo la serikali kuua kampuni binafsi za mafuta bali ni kuingia katika ushindani wa biashara ya mafuta ikiwemo uagizaji wa mafuta kupitia mfumo wa pamoja wa uagizaji wa mafuta(BPPA),kudhibiti bei ya mafuta ,kuwa na takwimu za matumizi ya nishati hiyo pamoja na usambazaji kwa ujumla. 

Amesema kuwa wanatarajia kuzindua vituo vingine sita vya aina hiyo baada ya kuzindua vituo vingine viwili Musoma  mkoani Mara na Segera wilayani Handeni mkoani hapa. 

Aidha,amesema  kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo Shirika hilo litajenga vituo  vingine 100 katika maeneo mbalimbali nchini katika Halmashauri za Wilaya sambamba na ujenzi wa matenki makubwa ya kuhifadhia mafuta katika  mikoa mbalimbali hapa nchini.

Mkurugenzi  huyo aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Tanga,Dar es salaam,Morogogo,Dodoma,Mbeya na Isaka-Kahama kwa kushirikiana na Mamlaka  ya Bandari nchini(TPA) ili kuunguza msongamano wa wfanyabiashara kuchukua mafuta sehemu moja pamoja na kupunguza misongamano ya magari lengo likiwa ni kulinda miundombinu ya barabara. 

“TanOil inachukua kazi zote za iliyokuwa kampuni ya mafuta ya Copec sasa tunaingia rasmi katika biashara ya mafuta, lengo si kuziondoa kampuni binafsi za mafuta bali ni kuleta ushindani, kudhibiti bei, kuwa na takwimu sahihi za mafuta na kuagiza mafuta kwa ujumla (BPPA),” alisema. 

Kuhusu  ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima-Uganda hadi Chongoleani jijini Tanga,amesema kuwa baada ya kampuni ya Tullow kuwauzia hisa zao kampuni ya mafuta ya Total,sasa kampuni hiyo itamiliki hisa hizo kwa asilimia 66.7 na wamefikia muafaka na mradi utaanza mapema mwakani . 

Amefafanua  kuwa katika kipindi cha mwezi Juni,wataanza kutangaza zabuni za ujenzi wa mradi kwa kampuni mbalimbali,mwezi Desemba watapitia kampuni hizo ili  kujua gharama za mradi na ujenzi wa mradi huo utasimamiwa na Shirika la  Mafuta la Uganda(NOC),Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) na  kampuni ya CNOOC. 

“Ujenzi wa bomba la mafuta uliokuwa uanze ulikwamishwa na mazungumzo ya kodi kati ya kampuni za mafuta kwa hiyo kuanzia mwaka huu mwezi Jui tutaanza kutangaza zabuni hadi mapema mwakani kazi zitaanza,hivyo wananchi wa mkoani Tanga kupitia miradi ya TPDC changamkieni fursa za kiuchumi na biashara,”alisema. 
 

Akizungumza  wakati wa uzinduzi huo ,Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela aliwashukuru TPDC kwa kuanzisha vituo hivyo mkoani humo nawataka wananchi kutoa ushirikiano wa ulinzi katika vituo hivyo kutokana ni mali  ya serikali na kuwasisitiza kuanzisha shughuli za uwekezaji zaidi na kjipatia fursa za ajira kupitia miradi ya TPDC ikiwemo kufunguliwa vituo  vya mafuta,gesi na mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi(EACOP). 

Pia,  amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Daudi Mayeji kuharakisha mchakato wa taarifa ya tathmini ya eneo ambalo TPDC watajenga tenki kubwa la kuhifadhia mafuta ili wananchi walipwe fidia na  ujenzi uanze haraka. 

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amesema kuwa katika mradi wa bomba la mafuta(EACOP)wilaya hiyo inapitiwa  na bomba hilo kwa urefu wa kilometa 54,na eneo la kambi kubwa itakayojengwa Handeni lina ukubwa wa ekari 51 na tayari wananchi wa Misima wamekubali kuondoka kupisha ujenzi huo. 

Kuhusu ujenzi wa vituo vya mafuta vya TPDC,amesema wilaya hiyo ina maeneo mengi ya uwekezaji hivyo amekubali kutoa eneo popote pindi TPDC wakitaka kwa ajili ya ujenzi huo. Awali Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Handeni,Athumani Malunda aliwaomba TPDC kujenga  vituo vingine viwili kama hivyo wilayani humo katika maeneo ya Mkata na  Handeni mjini na kumtaka Mkurugenzi Mtendaji ikibidi kuwapa eneo. 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Handeni,Athumani Malunda akizungumza wakati wa uzinduzi huo
MKUU wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akizungumza wakati wa uzinduzi huo
AFISA wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga Gibson George akizungumza jambo kwenye uzinduzi huo
Sehemu ya wananchi wakifuatilia uzinduzi huo
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katika akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo kushoto ni Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),Dk James Mataragio,Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe na kulia ni Mwenyekiti  wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.