Habari za Punde

Umewahi kutumia pesa hizi?Kama umewahi hizi basi wewe ni kijana wa zamani au mtu mzima wa leo

Kabla ya kutumia shilingi hapa kwetu tulikuwa tukitumia Rupia na pesa(paisa) ambazo asili yake ilikuwa ni kutoka India. Na Rupia moja enzi hizo ilikuwa  ni pesa arubaini.

Ilipokuja kubadilishwa matumizi kutoka Rupia na kuletwa Shilingi na Senti alipokuja Muingereza. Shilingi moja ilikuwa ni senti 100.

Wenyeji  wa visiwa hivi wakaona isiwe taabu wakachukua vile vile kuwa shilingi ni pesa 40 kama ilivyokuwa Rupia. 

Kwa hivyo pesa 1 ni sawa na senti 2 unusu. Kwa hiyo senti 5 ikaitwa pesa 2, senti 10 ni pesa 4 n.k 

Kama wewe ni kijana mpe challenge mzazi wako kama anayo taaluma hii au ameisahau

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.