Habari za Punde

Wananchi watakiwa kulipa ada za Manispaa

Na Takdir Suweid, Wilaya ya Magharibi ‘’B’’      
Afisa Manunuzi kutoka Baraza la Manispaa Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ Nunuu Ali Abdallah amesema kuna umuhimu mkubwa wa Wananchi kulipia  ada na ushuru unaotolewa na Mabaraza ya Manispaa ili yaweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Ameyasema hayo huko Fuoni mambosasa wakati alipokuwa  akizungumza na Wananchi kuhusiana na ulipaji wa ada.
Amesema Baraza hilo linakusanya ada za Wananchi katika leseni,Maduka,Taka na baadae kuzirudisha kwa kuwapelekea maendeleo Wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo ya njia za ndani, Umeme, Maji, Vituo vya Afya na Skuli za Maandalizi na Msingi.
Hivyo ni vyema kwa Wananchi kushirikiana na Baraza hilo katika kulipia Kodi ili kuweza kufikia malengo yaliowekwa na Serikali.
Aidha amewataka Makarani wanaokusanya pesa kuwa Makini na Waadilifu ili kuhakikisha Mapato ya Serikali hayapotei.
Kwa upande wake Diwani wa Wadi ya Fuoni Mambosasa Halima Salum Abdallah ameahidi kushirikiana na Uongozi wa Shehia katika kuhamasisha na kuandaa Sheria ndondogo zitakazowatia hatiani Wananchi watakaokwepa kulipa kodi katika ngazi ngazi ya Shehia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.