Habari za Punde

Matayarisho ya kuuaga Mwili wa Marehemu Rais Mstaafu Marehemu Benjamin William Mkapa

 Mafundi wakiendelea na harakati za kukamilisha matayarisho ya Uwanja wa Taifa kwa ajili ya shughuli za kuuaga Mwili Wa Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Tatu Marehemu Bendjamin William Mkapa
 Baadhi ya wapambaji wa maua wakikamilisha kazi ya upambaji wa jukwa litakalowekwa Mwili wa Mwili Wa Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Tatu Marehemu Bendjamin William Mkapa aliyefariki Dunia Usiku wa kuamkia Ijumaa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Matayarisho ya Mazishi ya Marehemu Mzee Bendjamin Mkapa Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa akiwa sambamba na Makamu Mwenyekitiwa Kamati Hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakitoa maelekezo walipofika Uwanja wa Taifa kuangalia hatua iliyofikiwa ya Matayari ya shughuliza Kuagwa Mzee Mkapa.
Kulia ya Mh. Majaliwa ni Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa anzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed na kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mh. Jenista Muhagama.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na Othman Khamis, OMPR
Matayarisho ya mwisho yanayofanywa na Serikali katika Uwanja wa Michezo wa Uhuru Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutoa nafasi kwa Viongozi, Wananchi pamoja na Wanadiplomasia kuuaga Mwili wa Marehemu Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu ya Jahumuri ya Muungano wa Tanzanzia Marehemu Bendjamin William Mkapa yameshafikia hatua za mwisho kukamilika.
Serikali Kuu imeandaa utaratibu huo Maalum ili kuwapa fursa Wananchi Kuuaga Mwili wa Kiongozi wao hasa ikizingatiwa Utamaduni na Heshima iliyojengeka kwa Watanzania kutoa Heshima kwa Viongozi wao waliotangulia mbele ya Haki kuwaaga baada ya kazi kubwa waliyoitekeleza kulitumikia Taifa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mazishi hayo Wazirri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Kassim akiambatana na mwenzake Makamu Mwenyekiti  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi walipata fursa ya kukagua Maandalizi hayo na kuridhika na hatua kubwa iliyofikiwa chini ya Watendaji wa Serikali waliopewa jukumu hilo.
Mwili wa Marehemu Mzee Mkapa aliyefariki Dunia Ghafla Usiku wa kuamkia Ijumaa utawekwa Uwanjani hapo kuanzia asubuhi ya Kesho Jumapili hadi Jumanne kwa shughuli hiyo ya kuagwa na Jumatano utapelekwa Kijiji chake Lupaso Masasi Mkoani Lindi kumalizia ambapo Alhamis Mchana utazikwa rasmi kwa heshima zote za Kitaifa.
Akizungumza na Watendaji wa matayarisho hayo Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi Kitaifa Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Kassim alisema lengo la Marehemu Mzee Mkapa kuzikwa Kijijini kwao nyakati za mchana limezingatia uhaba wa nyumba za kulala wageni ambapo waomnbolezaji watapa muda wa kurudi Mikoani mwao mapema.
Mh. Majaliwa alisema Kamati ya itaifa ya Mazishi imepanga utaratibu kwa kuwawekea muongozo Viongozi wa Kitaifa na wale wa Kidiplomasia kutoa heshima zao katika uwanja wa Taifa kwa lengo la kupunguza msongamanop wakati wa mazishi Mkoani Lindi.
Alisema Viongozi wa Mataifa mbali mbali Duniani wanaendelea kutoa salamu za rambi rambi kwa Tanzania kufutia kifo hicho na kufafanua kwamba Wale Viongozi wa Kimataifa watakaopata fursa ya kushiriki tukio hilo watapatiwa kutoa salamu Maalum kwenye shughuli hiyo ya kuuaga Mwili wa Marehemu.
Naye kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliipongeza Timu hiyo iliyopewa jukumu na kufanya matayarisho hayo na kusema kwamba jitihada zao zimewezesha kufanikisha maandalizi hayo kwa asilimia kubwa.
Balozi Seif alishauri kwamba zile kazi ndogo ndogo zilizobakia ni vyema kwa wahandisi na watendaji hao wakahakikisha kwamba zinakamilika kabla ya kufikishwa kwa Mwili wa Marehemu kuanza harakati za Kuuaga Mwili wake shusghuli zitakazoanza nyakati za asubuhi.
Marehemu Mzee Bendjamin William Mkapa ataendelea kukubukwa na Watanzania walio wengi hasa kutoka na Falsafa yake ya Ukweli na Uwazi iliyochangia na kumpa fursa ya kupambana na ufisadi pamoja na usimamizi wa Utawala Bora mambo yaliyopanua masuala ya Dedmokrasia Nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.