Habari za Punde

Uzinduzi wa Msikiti wa Kisasa wa Masjid Tauhid Fuoni Wilaya ya Magharibi "B" Unguja

Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislam wakati wa hafla ya Uzinduzi wa  Msikiti wa Masjid Tauhid  uliojengwa  upya  kupitia Mfadhili kutoka Nchini Oman. ukiwa na ghorofa moja na una uwezo wa kuchukua Waumini 300 kwa wakati mmoja katika Ibada ya Sala.
Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Masjid Tauhid Fuoni wakati wa ufunguzi wa Masjid hiyo uliofanywa na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mohmoud Mussa Wadi, kwa niaba ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Masjid Tauhid Fuoni Sheikh Suweid Ali Suweid, akitowa maelezo ya kufanikisha ujenzi wa Msikiti huo wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Masjid hiyo.
Katibu  Mtendaji wa Mali ya Amana na Wakfu Zanzibar Sheikh Abdalla Talib akitowa nasaha kwa Waumini wa Dini ya Kiisla wakati wa hafla ya ufunguzi wa Masjid Tauhid Founi Wilaya ya Magharibi "B" Unguja.
Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Khalid Ali Mfaume akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Masjid Tauhid Founi, uliofanyika juzi.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.