Habari za Punde

WAZAZI WATAKIWA KUKAMILISHA HUDUMA ZA CHANJO KWA WATOTO WAO

Mkurugenzi kinga na elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohammed Abdallah akifungua Semina ya siku moja ya wandishi wa habari wa Zanzibar ya Mpango wa chanjo katika ukumbi wa IRCH Kidongochekundu Mjini Zanzibar.

Na Ramadhani Ali - Maelezo 
Mkurugenzi Idara ya Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohammed Abdalla ameishauri jamii kuchukua jitihada zaidi kwa watoto wao kuhakikisha wanapata huduma ya chanjo kwa ukamilifu.
Amesema uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya wazazi na walezi hawakamilishi chanjo kwa watoto wao bila ya kujua kuwa kitendo hicho kinaweza kudhoofisha afya zao.
Dkt. Fadhil alitoa ushauri huo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja ya waandishi wa habari kutoka vyombo vya Zanzibar katika ukumbi wa Kitengo cha Huduma ya Mama na Mtoto (IRCH) Kidongochekundu.
Alisema mkakati wa huduma za chanjo umesaidia sana katika kuimarisha afya za watoto na kupunguza ama kuondosha kabisa baadhi ya maradhi yanayowasumbua.
Aliongeza kuwa mzazi anapompatia mtoto wake chanjo kamili anapunguza gharama ya matibabu na hupata nafasi ya kufanya shughuli za maenmdeleo kwa vile baadhi ya maradhi hayawezi kumsumbua .
Alikumbusha chanjo kwa Zanzibar inatolewa bure kinyume na nchi nyengine ambazo huduma hiyo hutolewa kwa malipo hivyo amewataka wananchi kuitumia fursa hiyo inayotolewa na Serikali na wafadhili ili kuwalinda watoto na maradhi yanayotibika kwa njia hiyo.
Alisema chanjo inasaidia kupata viongozi na wafanyakazi wenye afya bora kwani baadhi ya maradhi yanayowasumbua wakati wakiwa wadogo yanadhibitiwa na kukua vizuri wakiwa na afya bora.
Wakizungumzia hali halisi ya huduma za chanjo Tanzania Bara na Zanzibar, Afisa wa Mpango wa chanjo Taifa Dkt. Furaha Kyes na Mratibu wa chanjo Zanzibar Yussuf Makame walisema lengo ni kuepusha vifo vinavyotokana na magonjwa ambayo yanatibika kwa chanjo
Walisema Tanzania inaendelea kufanya vizuri katika huduma za chanjo na kila mwaka idadi ya watoto wanaopatiwa huduma hiyo imekuwa ikiongozeka kwa asilimia kubwa Tanzaina Bara na Visiwani.
Hata hivyo walisema chanjo dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi (HPV) inayotolewa  kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 kupitia maskulini, imekuwa na changamoto hasa wakati wa kipindi cha Corona kwani skuli zilikuwa zimefungwa na huduma hiyo ilisimama.
Baadhi ya wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali Zanzibar wakimsikiliza Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Fadhil Mohammed Abdallah (hayupo pichani) alipokuwa akifungua Semina ya siku moja ya Mpango wa chanjo katika Ukumbi wa IRCH Kidongochekundu.
Mratibu wa huduma za chanjo Zanzibar Yussuf Makame akitoa tarifa ya hali ya chanjo Zanzibar katika Semina ya siku moja ya wandishi wa habari wa Zanzibar iliyofanyika IRCH Kidongo chekundu.
Baadhi ya wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali Zanzibar wakimsikiliza Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Fadhil Mohammed Abdallah (hayupo pichani) alipokuwa akifungua Semina ya siku moja ya Mpango wa chanjo katika Ukumbi wa IRCH Kidongochekundu.
Afisa kutoka Mpango wa Taifa wa Chanjo Dk. Furaha Kyesi akisisitia umuhimu wa  chanjo katika kuwalinda watoto katika Semina ya wandishi wa habari wa Zanzibar iliyofanyika Ukumbi wa IRCH Kidongochekundu.
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohammed (alievaa koti) akiwa katika picha ya pamoja na wandishi wa habari na Maafisa kutoka Mapango wa Taifa wa chanjo Tanzania.
Picha na Makame Mshenga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.