Habari za Punde

WanaCCM watakiwa kusaidia kuzidisha upendo miongoni mwao

Na Takdir Suweid, Wilaya ya Mjini.       
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wametakiwa kuhurumiana na kusaidiana hasa katika kipindi cha Sikuu ya za Iddi ili kuzidisha Umoja na upendo miongoni mwao.
Katika Siku za Iddi imesisitizwa zaidi kutoa Sadaka,kusaidia Masikini, Mayatima na wasiojiweza ili na wao waweze kusherehekea kama Watu wengine.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Talib Ali Talib wakati alipokuwa akikabidhi Sadaka ya kitoeleo kwa Viongozi wa Chama hicho ngazi ya Matawi,Wadi,Majimbo,Wilaya na Mkoa wa Mjini huko Amani Wilaya ya Mjini.
Amesema kuna baadhi ya Wananchi wanaishi katika hali ngumu ya kimaisha hivyo Sadaka hiyo itawasaidia na familia zao kuweza kukabiliana na Sikukuu na kuwaomba Watu wenye uwezo kuwasaidia Wasiojiweza katika maeneo yao kadri hali itakavyoruhusu.
Nao baadhi ya Viongozi waliopatiwa Sadaka hiyo wamesema imeweza kuwasaidia na familia zao na kumuomba Mwenyekiti kuendeleza utaratibu huo kila mwaka inapofika Siku za Iddi ili uweze kuwasaidia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.