Habari za Punde

ZPTTA yataka wanahabari kushirirkiana nao kutangaza amani

Katibu mtendaji wa jumuiya ya Amani Ukweli na Uwazi Zanzibar (ZPTTA) Ali Mussa Mwadini akizungumza na  Wandishi wa habari na kuwataka washirikiane na jumuiya hiyo ili kulitangaza neno a amani,katika uzinduzi wa neno la amani hafla iliyofanyika ukumbi wa ZBC TV  (Karume House) huko Mnazimmoja mjini Zanzibar.

SABIHA KHAMIS – MAELEZO              
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Amani, Ukweli na Uwazi Ali Mussa Mwadini amesema anataka kuirejesha amani iliyopotea kwa Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla ili kuishi katika maisha ya amani ya kweli.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa ZBC TV wakati wa uzinduzi wa Jumuiya hiyo amesema dunia imepoteza utamaduni wa amani hivyo itafutwe mbinu ya kurejesha na kuleta maendeleo katika Taifa letu.
Aidha amesema hivi sasa dunia nzima mfumo wa amani tulionayo inakabiliwa na changamoto ya kupotea kwa utamaduni wa amani kwa mtu binafsi, familia, Taifa na hatimae dunia nzima.
“Dunia imeandamwa na ugomvi, vurugu na uvunjaji wa haki za binaadamu hii ni kwa sababu watu wanaishi katika misingi ya amani isiyo ya kweli” alisema Katibu huyo.
Amesema atahakikisha jumuiya hiyo itaijenga jamii ya Wazanzibar na wasio Wazanzibar waishio hapa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kuishi kwa usalama bila ya hofu wala kugopa katika misingi ya kujenga utamaduni wa kuaminiana.
Hata hivyo amesema amani ya kweli yenye kuleta mshikamano na maendeleo huanza ndani ya mioyo yetu ili kuifikisha jamii ya Wazanzibar kufikia kuishi kwa maisha ya amani.
Vile vile Katibu wa Jumuiya katika kutaja malengo amesema kuwa wameandaa mfumo maalum ambao utatekelezwa kwa mtindo wa mikutano ya nje ya kijamii kuanzia mashina hadi Taifa kwa muda wa mwaka mmoja Unguja na Pemba.
Pia amesema utekelezaji huo utawashirikisha wadau mbali mbali kama vile Vyombo vya Habari, wasanii, mitandao ya kijamii, wafanyabiashara na kampuni za simu vyote vikibeba ujumbe wa neno la amani hivyo kushirikiana kwa pamoja ili kulitangaza neno Hilo kwa jamii na wenye mahitaji maalumu.
Nae Mjumbe wa Jumuiya hiyo Mosi Ali Chako amsisitiza kuwa wamejipanga vyema katika kudhibiti vyanzo vyote vya uvunjifu wa amani ili kuhakikisha amani ya kweli inarudi kama zamani.
“Zamani watu waliishi kwaamani na upendo hakukuwa na mapigano, chuki, migogoro wala vurugu” alisema Mjumbe huyo.
Kauli mbiu ya Jumuiya ni ”Amani inaanza na mimi. Wewe je?”

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.