Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae na Mgombea Ubunge Jimbo la Mpendae Zanzibar Mhe. Salim Turky, akitambulishwa wakati wa uhai wake katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za CCM zilizofanyika katika Uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti jumamosi 12/9/2020 wiki iliopita.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae na Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Mhe. Salim Hassan Abdallah Turky (Mr. White) amefariki dunia jana usiki katika Hospitali ya Global Jijini Zanzibar
Kwa mujibu wa wawakilishi wa familia maziko yatafanyika leo 15/9/2020 nyumbani kwake Mpendae Jijini Zanzibar saa kumi baada ya sala ya Alasri na kusaliwa katika Masjid Noor Muhammad Kwa Mchina na anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Fuoni Kijitoupele.
Inshaalah Mwenyenzi Mungu ampe kauli thabi na kumsamehe madhambi yake
Ameen.
Inna Lillah wa Inna IIayhi Rajiuun
No comments:
Post a Comment