Habari za Punde

Mkutano wa Wadau wa Maradhi Yasioambukiza Zanzibar.


Mratibu wa Maradhi yasioambukiza Omar Abdalla Ali akitoa maelezo kuhusu ongezeko la Maradhi yasioambukiza huko katika Ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe.
Baadhi ya Wadau wa Mkutano wa Maradhi yasioambukiza wakifuatilia majadiliano ya Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe .
PICHA NA KHADIJA KHAMIS- MAELEZO ZANZIBAR.

Na.Khadija Khamis  –  Maelezo  Zanzibar 11/09/2020.
Imeelezwa kuwa jamii kuacha kutumia vyakula vyao vya asili na kuelekea zaidi vyakula vya makopo ni miongoni mwa sababu za kuongezeka kwa maradhi yasioambukiza nchini.
 Mkuu wa Kitengo cha Maradhi ya Kisukari Dk Faiza Kassim Sleiman  alisema huko katika ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe  wakati  wa Mkutano wa Wadau wa maradhi hayo.
Alisema kubadilika kwa mfumo wa maisha na wananchi kula chakula bila mpangalio imeleta changamoto kubwa ya maradhi yasioambukiza ambayo yamekuwa yakipoteza maisha ya watu wengi hivi sasa.
Akitoa ufafanuzi katika majadiliano yaliyokuwa yakiendelea katika mkutano huo wa wadau wa maradhi yasioambukiza, aliwashauri kupunguza matumizi ya vyakula vya makopo ambavyo haviimarishi afya zao.
Aliwashauri kutumia zaidi matunda na mboga mboga na kutilia mkazo katika kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao.
Mratibu wa Maradhi yasiyoambukiza Omar Abdalla Ali alieleza hatua zinazochukuliwa ni pamoja na kutoa elimu na ushauri kwa jamii ambayo yatasaidia kuwa kila watu milioni 40 waliokufa asilimia 70 ni wa maradhi yasiyoambukiza .
 Kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika  Zanzibar mwaka 2011 zilionyesha kati ya watu 100, 33 wamegunduliwa na maradhi yasioambukiza wenye umri wa miaka 25 hadi 69 .
Akiyataja maradhi  yasioambukiza ambayo yanaongoza zaidi kuadhiri ni ugonjwa wa kisukari, shindikizo la damu,Saratani ya Shingo ya kizazi,Saratani ya Tenzi Dume, Saratani ya Matiti,, Ajali za Barabarani pamoja na Matatizo ya Meno .
Zaidi ya Akinamama 12,212 waliofika kushunguzwa saratani ya shingo ya kizazi katika Hospitali ya Rufaa Mnazimmoja,Akinamama 371, sawa na asilimia tatu waligunduliwa na saratani ya shingo ya kizazi  na 34 walipelekwa Ocean Road kwa matibabu zaidi.
Nae Dk Suleiman Selele Mratibu wa Tamasha la  Vyakula vya Asili linalofanyika Makunduchi alisema ushirikishwaji wa jamii katika masuala ya kiafya utasaidia utumiaji wa vyakula vlivyo sahihi ambavyo havina vichocheo cha maradhi yasioambukiza .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.