Habari za Punde

Mkutano wa Kampeni Mgombea Urais wa Zanzibar Kwa Tiketi ya CCM Mhe. Dk Hussein Mwinyi Uwanja wa Jamuhuri Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja leo 1-10-2020.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi alipowasili katika Jukwaa Kuu la Viongozi kuhudhuria mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar uliofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja leo 1/10/2020. 
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibare ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais Mstaaf wa Tanzania Awamu ya Pili Mhe Ali Hassan Mwinyi alipowasili katika Jukwaa kuu la Viongozi Uwanja wa Jamuhuri Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, kuhudhuria mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein  Mwinyi.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akisalimiana na Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi alipowasili katika Jukwaa juu la Viongozi Uwanja wa Jamuhuri Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja leo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduziu Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na Viongozi wa Jukwaa Kuu la Viongozi wakiwa wamesimama wakati wakiimba wimbo ya Ukombozi kabla ya kuaza kwa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Mwinyi ulionyika leo uwanja wa Jamuhuri Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe Ali Hassan Mwinyi akiwa na Viongozi wakiwa wamesimama wakati wakiimba wimbo wa ukombozi katika hafla ya Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Mwinyi uliofanyika katika Uwanja wa Jamuhuri Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja leo. 
Wanachama wa Cha Cha Mapinduzi wakiwa na bango la picha za Wagombea Urais wa Zanzibar Mhe. Dk .Hussein Mwinyi na Mgombea wa Urais wa Tanzania Mhe John Magufuli, wakati wakiimba wimbo wa ukombozi katika uwanja wa Jamuhuri Makunduchi wakati wa hafla ya mkutano wa Kampeni wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja uliofanyika leo.
Team Mwinyi Kwanza wakiwa na bango la picha ya Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Dk. Hussein Mwinyi na picha yao wakiwa katika mmoja ya mikutano ya kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar uliofanyika Nungwi hivi karibuni , wakiimba wimbo wa ukombozi. katika mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar uliofanyika katika Uwanja wa Jamuhuri Makunduchi leo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiri Ally wakiwa katika uwanja wa mpira wa Jamuhuri Makunduchi wakihudhuria mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Dk. Hussein Mwinyi uliofanyika leo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduziu Dkt. Bashiri Ally akihutubia katika hafla ya Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Urais wa Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Jamuhuri Makunduchi Mkoa wa Kusinu Unguja leo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar ambae poia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akihutubia katika mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar uliofanyika katika Uwanja wa Jamuhuri Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja na kumuombea Kura kwa Wananchiu wa Mkoa huo pamoja na Wabunge,Wawakilishi na Madiwani wa CCM.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Mwinyi akihutubia Wananchi wa Mkoa wa Kusini na kutangaza sera zake wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Jamuhuri Makunduchi na kuwaiombea Kura.  
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.