Habari za Punde

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jaji Mkuu Mstaaf Hamid Magmoud Hamid Akitangaza Matokeo ya Uchaguzi wa Rais wa Zanzibar.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji Mkuu Mstaaf wa Zanzibar Mhe Hamid Mahmoud Hamid  (katikati) akitangaza matokeo ya Kura za Rais wa Zanzibar baada ya kumalizika kwa zoezi la upigaji Kura uliofanyika Zanzibar kumchagua Rais wa Zanzibar na Wawakilishi  na Madiwani, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa kuhesabia kura na kutangazwa matokeo katika Chuo cha Utalii Maruhubi Jijini Zanzibar. matokea hayo yametangazwa jana jioni 29/10/2020. 
Wagombea Urais wa Zanzibar wakifuatilia matangazo ya kutangazwa mshindi wa Urais wa Zanzibar baada ya kumalizika zoezi la Upigaji kura Zanzibar, hafla hiyo ya kutangazwa matokeo imefanyika katika ukumbi wa majumuisho ya Kura Maruhubi Chuo Cha Utalii Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe. Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi akiwa na Wagombea Urais swa Vyama vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wakifuatilia matokeo hayon yakitangazwa katika ukumbi wa kujumlishia kura na utoaji wa matokeo Chuo cha Utalii Maruhubi Jijini Zanzibar. 
Waangalizi wa Ndfani wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wakifuatilia matokeo ya Uchaguzi wa kura za Urais wakati Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji Mkuu Mstaaf  wa Zanzibar Mhe Hamid Mahmoyud Hamid (hayupo pichani) hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa kujumlishia kura Chuo cha Utalii Maruhubi Jijini Zanzibar.


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.