Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi Akijumuika na Wananchi Katika Maziko ya Marehemu Iddi Mohammed Bavuai Maisara Jijini Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika Sala ya kuusalia Mwili wa Marehemu Iddi Mohammeed Bavuai iliofanyika katika Msikiti wa Maisara leo adhuhuri na kuzikwa Kijiji kwao Shakani Wilaya ya Magharibi "B" Unguja Mkoa wa Mjini Magharibi. 
Sheikh Aliyani akisoma dua kumuombea Marehemu Iddi Mohammed Bavuai baada ya kumalizika kwa Sala ya kumsalia marehemu iliofanyika katika Msikiti wa Maisara Jijini Zanzibar leo baada ya Sala ya Adhuhuri na kuzikwa katika makanuri ya kijijini kwao Shakani Zanzibar. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Waumini wa Kiislam baada ya kumalizika kwa Sala ya kumuombea Marehemu Iddi Mohammed Bavuai iliofanyika katika Msikiti wa Maisara Jijini Zanzibar  baada ya Sala ya Adhuhuri na kuzikwa katika makaburi ya Shakani Kijijini kwao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kumfariji Mtoto wa Marehemu Mohammed Iddi, baada ya kumalizika kwa Sala ya kumuombea Marehemu Iddi Mohammed Bavuai iliofanyika katika Msikiti wa Maisara Jijini Zanzibar  baada ya Sala ya Adhuhuri na kuzikwa katika makaburi ya Shakani Kijijini kwao.


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.