Habari za Punde

Makamu wa Rais Mhe Samia arejea nchini leo akitokea Botswana

Na Mwandishi wetu 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amerejea Nchini leo Novemba 28,2020 akitokea Jijini Gaborone Nchini Botswana alipohudhuria mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Kusini mwa Afrika SADC.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan,aliondoka Nchini Juzi kwa ajili ya kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa dharura wa pamoja baina ya SADC,  ORGAN TROIKA Nchi zinazochangia vikosi vya Ulinzi na Amani vya Umoja wa Mataifa uliokutana kwa dharura kuangalia hali hali ya matishio ya kigaidi ambapo katika kipindi hiki kumekuwa na matishio ya kiusalama katika Nchi ya Msumbiji, Congo DRC lakini pia na Tanzania.

Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Nchi za Wanachama wa Jumuiya ya Kusini mwa Afrika, pia uliangalia mapendekezo mapya ya mfumo wa Ulinzi katika eneo la DRC ambapo Nchi tatu zinazoshiriki katika shuhuli ya kuweka Usalama na Ulinzi ikiwemo Tanzania, Malawi na Afrika ya Kusini kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa umetoa mapendekezo mapya ya mfumo ambao utaweka Ulinzi bora na Usalama ndani ya DRC.

Aidha mkutano huo umeangalia hali halisi ya Usalama ndani ya eneo la Nchi Jumuiya ya Kusini mwa Bara la Afrika jinsi ya kutumia Usalama ulipo kwa ajili ya kujenga Uchumi Imara kwa Wananchi wa Nchi zilizo ndani ya Jumuiya hiyo,  ambapo pia mkutano huo kupitia Mwenyekiti wake Rais wa Botswana Dkt. Mokgweetsi Erick Eabetswe Masisi umeipongeza Tanzania Hususan Chama cha Mapinduzi CCM kwa kuweza kufanya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kwa salama na Amani.

Kwenye mkutano huo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, alioambatana na baadhi ya Viongozi wa Serikali akiwemo Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Aidan Kabudi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.